Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Dar
Askofu Mkuu wa KKKT Azania Front,Dkt. Alex Malasusa, ameongoza ibada ya misa takatifu ya kumuaga aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Ngoyai Lowassa leo Jijini Dar es Salaam, huku akiwataka watanzania kuyatumia maisha yake ya kiroho kama funzo.
Askofu Dkt. Malasusa amesema ni vyema kujitafakari katika kipindi hiki cha uhai kwa kuyaishi yanayompendeza Mungu kwa ajili ya kupata mwisho mwema.
“Huu siyo wakati wa kuendelea kuomboleza badala yake mtafakari zaidi Mungu..ndugu yetu Edward Lowassa alikuwa ni mcha Mungu, wakati akiwa na afya njema hakuwahi kuacha kufika hapa kanisani kwenye ibada na hivi ndivyo tunavyotakiwa kuishi kwa kujifunza kupitia maisha yake”, amesema Askofu Malasusa.
Pia amesisitiza kuishi maisha ya kumjua Mungu wakati wote wakiwa hai.
Mwili wa Edward Lowassa utasafirishwa kesho kuelekea Monduli jijini Arusha kwa ajili ya mazishi Februali 17, Mwaka huu.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua