December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Askari polisi adaiwa kujiua kwa kujipiga risasi Mbeya

Na Esther Macha Timesmajira Online, Mbeya

Askari waJesho la Polisi Mkoa wa Mbeya J. 2596 Kostebo Samweli Kaziyote (24) wa kituo kikuu cha polisi Mbeya anadaiwa kujiua kwa kujipiga risasi kidevuni na kusababisha kifo chake.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema kuwa tukio hilo limetokea Octoba 2 mwaka huu majira ya saa 2.15 usiku huko maeneo ya mtaa wa Mzumbe Forest ya zamani.

Kamanda Kuzaga amesema kuwa askari huyo alijipiga risasi kidevuni na kusababisha kifo chake hapo hapo

Hata hivyo Kamanda Kuzaga amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni mzozo uliotokea baina yake na mpenzi wake baada ya marehemu kuacha lindo la benki kisha kuondoka na silaha hiyo kwenda nyumbani kwa mpenzi wake huyo na kujipiga risasi.

Hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.