December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt.Anna Makakala

Askari 3 waliomuadhibu “tapeli” wasimamishwa kazi

Na Joyce Kasiki, TimesMajira Online, Dodoma

IDARA ya Uhamiaji imewasimamisha kazi askari watatu wa ofisi ya Uhamiaji Kurasini mkoani Dar es Salaam kwa kosa la kutumia nguvu dhidi ya Alex Kyai anayedaiwa kuwa ni tapeli.

Akizungumza ofisi kwake jijini Dodoma Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt.Anna Makakala alisema askari hao wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa tukio.

Alisema Idara ya Uahmiaji inakiri kutokea kwa tukio hilo na inalaani kitendo kilichofanywa na askari hao kwa kutumia nguvu kinyume cha sheria na maadili ya kazi zao.

Akielezea kuhusu tukio lililofanywa na askari hao Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt.Makakala alisema,tukio hilo lilitokea Mei 27 mwaka huu ambapo Idara ya Uhamiaji ilimkamata mtuhumiwa utapeli Alex Raphael Kyai katika ofisi ya Uahamiaji Kurasini Dar es Salaam .

Alisema mtuhumiwa huyo alikuwa ameongozana na mteja wa huduma wa paspoti aliyemtamnilisha kama mkewe .

Hata hivyo baada ya mahojiano ilibainika kuwa mtuhumiwa huyo amebainika kuwa amekuwa na tabia ya kuwalaghai na kupokea fedha kutoka kwa wateja mbalimbali ili waweze kupata paspoti kwa haraka .

Pia alisema mtuhumiwa huyo amekuwa akijitambulisha kama mtuhumishi wa taasisi nyeti ikiwemo Taaisi ya Kuzuia na Kuoambana na Rushwa (TAKUKURU.)

Kufuatia tukio hilo Idara ya Uhamiaji inatoa wito kwa kwa wananchi wote wanaohitaji huduma za kiuhamiaji kufika wenyewe kwenye ofisi za Uhamiaji badala ya kutumia watu.