January 15, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Argentina, Brazil fainali ya kibabe Jumapili

BRASILIA, Brazil

TIMU ya Taifa ya Argentina imefanikiwa kutinga fainali ya Copa America kwa ushindi wa penalti 3-2, kufuatia sare ya goli 1-1 dhidi ya Colombia ndani ya dakika 120 mchezo uliofanyika Alfajiri ya jana kwenye Uwanja wa Brasília nchini Brazil.

Shujaa wa Argentina alikuwa kipa wa Aston Villa, Emiliano Martinez, aliyeokoa penalti tatu za Colombia.

Mshambuliaji wa Inter Milan, Lautaro Martinez alianza kuifungia Argentina dakika ya saba akimalizia pasi ya Nahodha wa timu hiyo, Lionel Messi, kabla ya mshambuliaji wa Porto, Luis Díaz kuisawazishia Colombia dakika ya 61 akimalizia pasi ya Edwin Cardona.

Kwenye mikwaju ya penalti wachezaji walioshinda ni, Lione Messi, Leandro Paredes na Lautaro Martínez huku Rodrigo De Paul pekee alikosa.Kwa upande wa Colombia waliofunga ni Juan Cuadrado na Miguel Borja huku Davinson Sánchez, Yerry Fernando Mina na Cardona walikosa.

kufuatia matokeo hayo, sasa Argentina itakutana na wenyeji, Brazil katika fainali ya Copa America Jumapili Uwanja wa Jornalista Mário Filho, au Maracana Jijini Rio de Janeiro.

Argentina Mabingwa mara 14 (wa pili kubeba mara nyingi katika historia), watakutana kwa mara ya nne kwenye fainali ya mashindano hayo dhidi ya Brazil Mabingwa mara tisa (wa tatu katika historia) na ndio mabingwa watetezi wa michuano.

Mara ya mwisho 2007, Argentina alipigwa goli 3-0 katika fainali huko Venezuela, kipigo cha pili mfululizo katika fainali mbele ya Brazil pia 2004 kwa mikwaju ya penati nchini Peru.