December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Anerlisa Mungai atoa ujumbe mzito

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

ALIYEKUWA mke wa msanii wa RnB Bongo, Benpol, Anerlisa

Mungai kutoka Kenya ametoa ujumbe mzito juu ya uhusiano

wake wa kimapenzi na staa huyo.

Akitoa ujumbe huo kupitia kwenye Ukurasa wake wa

Instagram Anerlisa ameandika; “Ukianza kitu, kuwa na

ujasiri wa kumaliza pia. Mimi siyo mama wa mtoto wa

mtu, kwa hivyo usifikirie unaweza kushikilia maisha

yangu,”

Wakati habari za talaka yao zilipoibuka, ilisemekana

kwamba Benpol ndiye aliyeanzisha taratibu za kudai

talaka.

Kupitia mitandao ya kijamii, mwanadada huyo amesema,

alichotakiwa kukifanya alishakifanya na ametia saini.

“Nataka kuweka mambo wazi kuwa nilisaini chochote

kilichohitajika kusainiwa, na sitamani kuhusishwa na

mtu yeyote mtazamo wangu hivi sasa, ni kazi yangu na

amani yangu,” amesema Anerlisa.