Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Vijana na Ajira Patrobass Katambi Alipotembelea banda la shirika la Amref Tanzania katika viwanja vya Ilulu mkoani Lindi, katika wiki ya maadhimisho kuelekea siku ya UKIMWI duniani. Kwa miaka zaidi ya thelathini (30) sasa, shirika la Amref limekuwa likishirikiana na serikali ya Tanzania pamoja na wadau wengine kuboresha mifumo ya afya nchini.Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Vijana na Ajira Patrobass Katambi akiwa katika banda la wasichana balehe na wanawake vijana (AGYW) waliochini ya program ya Global Fund Timiza Malengo na kujionea shughuli zinazofanywa na vijana hao katika viwanja vya Ilulu mkoani Lindi, katika wiki ya maadhimisho kuelekea siku ya UKIMWI duniani. Kupitia programu ya Global fund wasichana balehe na wanawake vijana hunufaika na program hii kwa kupewa elimu ya mabadiliko ya tabia na kuanzishiwa miradi ya ujasiriamali ili kuepuka vishawishi vitakavyowaweka katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
More Stories
Kituo cha mfano Katente chaongeza makusanyo MBOGWE
Elimu ya fedha yawafikia wananchi wa Makanya wilayani Same
Wasira:Uchaguzi Mkuu utafanyika wanaCCM,Wananchi jiandaeni