December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

 AMO,yaipa tano, bodi ya filamu

Na Bakari Lulela, Timesmajira Online,Dar

MKURUGENZI wa taasisi ya Amo Foundation ya Dar-es-Salaam, Amina Saidi, amesema sanaa ni nyenzo muhimu katika kujenga afya na kufikisha ujumbe kusudiwa kwa haraka.

Akizungumza jijini Dar-es-Salaam katika uzinduzi wa tamasha la kimataifa, lililoandaliwa na Bodi ya Filamu,Amina amesema tasnia ya filamu ni muhimu katika kufikisha ujumbe kwa jamii kwa haraka.

Pia ameeleza kuwa ni hatua kubwa imeweza kufikiwa na tasnia ya filamu kwa kuwakutanisha wadau mbalimbali wa filamu ambapo sanaa ni bora katika kuendeleza utamaduni wa Mtanzania.

Sanjari na hayo ameeleza kuwa,taasisi hiyo inasaidia vijana kwa kutoa mafunzo na kozi mbalimbali,kisha kuwapa vifaa, mtaji au fedha kwa ajili ya shughuli tofauti.

Katika uzinduzi huo wadau wa sekta ya sanaa pamoja na wasanii mbalimbali,walishiriki katika kuendeleza utamaduni wa mwafrika unaosambaa zaidi kupitia ujumbe wa filamu.