January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Amber Rutty, mumewe, James Delicious kutumikia miaka mitano jela

Na Grace Gurisha, TimesMajira Online

MSANII Rutyfiya Abubakary maarufu kama ‘Amber Rutty’, aliyekuwa mume wake Said Bakary pamoja James Charles maarufu kwa jina la James Delicious wameanza kutumikia kifungo cha miaka mitano baada ya kushindwa kulipa faini waliyopangiwa.

Amber Rutty na wenzake wamepekwa gerezani baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwamuhukumu kulipa faini ya Sh. Milioni 11 au kutumikia kifungo cha miaka mitano jela, baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Mbali na Amber Rutty na Bakary mshtakiwa mwingine aliyehukumiwa katika kifungo hicho ni James Charles maarufu kwa jina la James Delicious, ambaye na yeye amepatikana na hatia katika makosa matatu yanayowakabili.

Hukumu hiyo ametolewa na Hakimu Mkazi Mfawishi wa Mahakama hiyo, Godfrey Isaya, baada ya kujiridhisha na ushahidi wa upande wa mashtaka kuwa washtakiwa walitenda makosa hayo.

Wakati anatoa hukumu hiyo, Hakimu Isaya amesema, amezingatia hoja za pande zote mbili na athari za makosa hayo, kwa sababu ni kweli washitakiwa wote ni vijana na wanategemewa katika jamii.

“Nimeona mshtakiwa wa kwanza anajutia kosa lake, wa pili na tatu ni wakosaji wa kwanza, kutokana na mazingira ya kesi hii adhabu yake ni miaka 30 kila kosa ambapo nikiwafunga mtapotea kabisa,” amesema Hakimu Isaya

Kutokana na mazingira waliyoyasema na lengo la adhabu ni kujirudi, basi mshtakiwa wa kwanza atalipa Sh Milioni tatu au kwenda jela miaka mitano.

Mshtakiwa wa pili atalipa faini ya Sh. Milioni tatu au kwenda jela miaka mitano na mshtakiwa wa tatu pia atalipa faini ya Sh. Milioni tano au kwenda jela miaka mitano, ambapo adhabu zitaenda sambamba, kwa hiyo washtakiwa watatumikia kifungo cha miaka mitano jela kila mmoja.

Katika hukumu hiyo, hoja kuu zilikuwa saba, ikiwemo kama mshtakiwa Amber Rutty ndiye aliyeonekana katika video ya ngono ama lah, pia kama mshtakiwa huyo ameingiliwa kinyume na maumbile ama lah, pia kama mshtakiwa Said alimuingilia kinyume Amberutty .

Hakimu Isaya amesema kuwa, baadhi ya hoja hazikuwa na shaka ikiwemo iliyomuhusu mshtakiwa Amberutty ambaye alipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na kufanyiwa vipimo sehemu ya nyuma na kubaini kupo wazi.

Katika hukumu hiyo, Hakimu Isaya amesema upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi 10, huku upande wa utetezi wakijitetea washitakiwa wenyewe.

Kabla ya Hakimu Isaya, kusoma adhabu hiyo, Wakili wa Serikali, Faraja Ngukah aliieleza mahakama kuwa, hakuna rekodi za makosa ya nyuma, kutokana na makosa waliyotiwa nayo hatiani ni makosa ambayo yamezuiliwa hata na vitabu vitukufu, kwa hiyo tunaomba adhabu stahiki ili iwe fundisho.

Baada ya Wakili Ngukah kudai hivyo, Amberutty aliomba apunguziwe adhabu kwa sababu ana watoto wanamtegemea na mmoja anamatatizo ya ugonjwa wa pumu, ana wazazi wanamtegemea na pia anaugua ugonjwa wa TB.

“Naiomba mahakama isinipe adhabu kali mimi ni mtoto mkubwa ninayetegemewa na familia, mama yangu amezeeka na ninasumbuliwa na TB natumia vidonge, mahakama inionee huruma,” amesema Bakary wakati anajitetea asipewe adhabu kubwa 

Mshtakiwa Charles kupitia wakili wake , ameiomba Mahakama ipunguzie adhabu kwa sababu haijawahi kutiwa hatiani wala rekodi ya jinai. 

Katika kesi hiyo kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile lilikuwa linamkabili Amber Rutty, ambapo anadaiwa amelitenda kati ama baada ya Oktoba 25, 2018 ambapo alimruhusu Bakary kumuingilia kinyume na maumbile.

Katika shtala lingine ni kufanya mapenzi kinyume na maumbile, linamkabili mshtakiwa wa pili Bakary, adaiwa kati ama baada ya Oktoba 25,2018 jijini Dar es Salaa alifanya mapenzi na Amber Rutty kinyume na maumbile.

Kosa la tatu la kuchapisha video ama picha za ngono, ambapo linamkabili James Charles ama James Delicious akidaiwa kati ya October 25,2018 alisambaza video za ngono kupitia magroup ya Whatsapp.