Na Penina Malundo,TimesMajira Online
KESHO Oktoba 28,2020 Watanzania wanaingia katika historia nyingine ya kuwachagua viongozi wa nafasi ya urais,wabunge,madiwani na Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Takribani miezi miwili sasa imekatika viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa wamekuwa wakinadi sera kwa wananchi juu ya kitu ambacho watakifanya baada ya kuchaguliwa ndani ya kipindi cha miaka mitano.
Hii ni fursa pekee ya Watanzania kufanya uchaguzi huo kwa hali ya amani, upendo na ushirikiano bila kutokea kwa vurugu zozote zitakazosababishwa na mtu mmoja au kikundi cha watu.
Uchaguzi huo usiwe ni sababu ya kuvuruga umoja na mshikamano wa kitaifa, lakini zaidi amani ambayo ni chachu ya maendeleo fungamani ya binadamu.
Ikumbukwe kuwa muasisi Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere kwa maono ya tunu tano alizoziacha nchini na kuwahakikishia Watanzania kuzisimamia ipasavyo ni pamoja na kutunza amani,umoja na mshikamano kwa lengo la kuepuka suala la udini na ukabila katika nchi ambayo inaweza kuigawa nchi vipande vipande.
Hayati Mwalimu Nyerere alikuwa mtu wa pekee na sio kwa Tanzania tu bali ni kwa bara la Afrika na duniani kwa ujumla kwani alikuwa kiongozi shupavu, ,jasiri,mwenye maono,mwanamapinduzi,mwafrika halisi,mpendam amani,umoja, mtetezi wa wanyonge hali ambayo mataifa mengi walikuwa wanapenda kumtumia.
Hivi karibuni nchi imefanya kumbukizi yake ya kufikisha miaka miaka 21 tangu kufariki dunia,hivyo tunapoelekea katika Uchaguzi huu Mkuu Watanzania wanapaswa kukumbuka tunu alizoziacha Mwalimu Nyerere kwa kuhakikisha amani ya nchi inatuzwa na kutovurugwa na watu wa aina yoyote kwa sababu ya uchaguzi.
Katika uhai wa Mwalimu Nyerere Akizungumzia aliipigania amani ndani na nje ya mipaka ya nchi ya Tanzania,hata mauti ilipomkuta mwaka 1999 alikuwa msuluhishi wa mgogoro nchini Burundi .
Ni ukweli usiopingika amani ya nchi inaweza kutoweka kwa siku moja ila kurudisha amani hiyo itachukua muda mrefu ni vema Watanzania kukaa na kutafakari kuchuja maneno ya wagombea na kuona yapi yanayofaa kwa muda sahihi wa kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu.
Rais John Magufuli ambaye pia ni mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),anasema Watanzania wanapaswa kuwakataa viongozi wanaotaka kupoteza amani ya nchi na kukumbuka kuwa amani ikitoweka Watanzania hawatakuwa na mahali pa kukimbilia kwa sababu hata nchi jirani zinategemea Tanzania.
Anasema endapo amani itatoweka watakaoathirika ni watoto,akinamama na wazee hivyo ni vema kutunza amani iliyopo wengi wenye nia ya kuchochea vurugu wana mahali pa kukimbilia.
“Wakati huu wa uchaguzi ni wakati wa kuamua kama wananchi wanataka maendeleo,amani,upendo au vurugu,”anasema na kuongeza
“Oktoba 28,2020 siku ya Jumatano ni jukumu la wananchi kuamua,Tanzania imekuwa taifa kubwa ambalo limetoka katika uchumi wa chini na kuingia uchumi wa kati ambapo imetengeneza maadui wengi,”anasema.
Anasema nchi ya Tanzania katika uchumi wake ni miongoni mwa nchi 10 zilizo na uchumi wa juu kwa nchi za Afrika.
“Tanzania ina mali kila mahali,watu wanameza mate na watafurahi siku moja wakiona Watanzania watakapoanza kupigana wao watakuja kutuuzia silaha huku wakichimba dhahabu ,Almasi na Tanzanite…mkimaliza kupigana mnakuta wamemaliza kuchukua mali zote zilizopo,”anasema.
Aidha Magufuli anasema hata siku ya kupiga kura kuna watu wamepanga kuwazuia akinamama na kuwatisha wasiende kupiga kura.
“Mkinichagua kwa miaka mingine nataka kuitunza amani na usalama wa Watanzania wote,nataka nchi hii iendelee kuwa kisiwa cha amani.
“Msifikiri watu wanaopigana hadi leo wanapenda vita,ukichezea amani ni kama unachezea yai,ukiangusha chini yai likipasuka huwezi kuunganisha tena ,ni kama tunu tuliyoachiwa na waasisi ni vema amani tuliyonayo tuitunze na kuiendeleza,”anasema.
Magufuli anasema ukichezea amani leo ikipotea kuirudisha ni miaka 200 na
hata yule aliyeichokoza amani hiyo na kusababisha mfarakano na yeye hatopona.
Magufuli anasema anayezungumzia suala la maandamano lengo lake ni kuharibu amani ya nchi iliyotengenezwa na hayati Mwalimu Nyerere kipindi cha muda mrefu.
Anasema amani ya nchi inapaswa kulindwa na Watanzania wote kwani ni vema kutambua kuna maisha baada ya kufanyika kwa uchaguzi,Watanzania wanawajibu kujiona kama ndugu na kuwa pamoja katika kulipenda taifa .
“Maisha sio kuwa rais,mbunge au kuwa nani,tunapongombea nafasi hizi ni nafasi ya wananchi wenyewe kupima mtu gani wanamtaka na wanamfahamu kwa kipindi hiki.
“Mwaka 2015 tulikuwa na mgombea wa ACT-Wazalendo mama Anna Mwingira alikuwa anagombea nafasi ya urais lakini katika kampeni zake zilikuwa za kiistaarabu na haukuweza kusikia anamtukana mtu na alikuwa anazungumzia sera ya chama chake na ndio maana tulipomaliza nikamteua kuwa mkuu wa Mkoa wa Moshi.
“Yupo Prof.Mkumbo hakuwa CCM,nilimteua kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na wengine wengi,hata Lowasa alipohamia upande mwingine hakututukana ndio maana yalipomzidia kule alirudi huku tukamkaribisha ila angetutukana nisingempokea pia yupo Balozi Dkt.Willibroad Silaa naye alikuwa upinzani lakini kampeni zake zilikuwa nzuri hadi nikamteua kuniwakilisha katika balozi wa nchi tisa ,”anasema Dkt.Magufuli
VIONGOZI WA DINI WAZUNGUMZIA AMANI
Asilimia kubwa ya viongozi wa dini nchini wamekuwa wakihubiri suala la amani katika nchi na kuwataka wauumini wao kuhakisha wanailinda amani iliyopo nchini.
Na viongozi hao wamekuwa wakisema kuwa wao wapo kwa ajili ya kuhubiri amani,upendo na mshikamano uliopo nchini na hawakubaliani na suala la lichezea amani iliyopo na hata hivyo hawaungi mkono chama chochote cha siasa.
Sheikh wa Mkoa Kilimanjaro,Mlewa Shaban anasema Mkoa wa Kilimanjaro hawapendelei chama chochote na hakuna makubaliano waliyoafikiana ya kuunga mkono chama fulani.
“Sisi viongozi wa dini mkoa wote wa Kilimanjaro tunayo kamati maalum inaitwa kamati ya mahausiano mbalimbali, katika kamati hiyo, tumefanya mengi tukiwa pamoja.Tumekubaliana kuwa sisi kilimanjaro hatukipendelei chama chochote, na hatujapeana maagizo yoyote.
“Mufti wetu ameshayasema haya mbele yako ukiwa mjini Korogwe, hatuna haja ya kusema tena,lakini tunasema kwa faida ya Watanzania kwamba endapo wakiona kwenye vyombo vya habari wakielekeza tumchague nani basi waelewe jambo hilo siyo kweli.
“Tunafahamu Serikali ilivyotutuza,mfano hospitali ya KCMC inavyotuhudumia katika hospitali hiyo kwa kupeleka dawa na kuwalipa madaktari, hivyo hatuwezi kusema kuwa tupo dhidi ya Serikali wala kwenda kinyume na Serikali kwani tunajua umuhimu wa serikali” anasema.
Naye, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili ya Kirutheri Tanzania (KKKT), Dkt.Fredick Shoo aliliombea Taifa kwa kutaka kudumisha amani anasema“Tunamshuru Mungu kwa kukuleta salama Rais Magufuli mkoani Kilimanjaro, tunafuraha kwa kukupokea, shukrani nyingi kwa Mungu”
“Tunamuomba Mungu akulinde kwa kipindi chote utakachokuwa Moshi na safarai yako utakapokuwa popote.Sisi wana Kilimanjaro na kwa niaba ya dini zote, tunapedna kufanya maombi kwa nchi yetu, kwako na watu wote. Mungu tuepushe na vurugu za aina zote, tukailinde amani, tuepushe na kutoelewana, majivuno, kiburi na maneno yanayochochea amani
More Stories
Hivi ndivyo TASAF ilivyoshiriki kumaliza kilio cha wananchi Kata Bwawani, Arusha
Mfumo unavyokwamisha wanawake kuwa viongozi
Mussa: Natamani kuendelea na masomo,nikipata shule ya bweni