November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

ALMTC kinara katika sekta ya Afya

Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha

Chuo cha Arusha Lutheran Medical center kilichopo Ekenywa mkoani kimefanikiwa kujiwekea utaratibu wa kuwafundisha wanafunzi wake kwa vitendo kupitia hospitali tano ili kuwafanya wanafunzi kuwa na uzoefu zaidi wa kuwasaidia jamii

Hayo yameelezwa mapema Jana na Mkuu wa ya Mafunzo na ubora kutoka katika hospitali ya selian Dr Godwill kivuyo wakati akiongelea mafunzo ambayo yanayoleta na chuo hicho kwenye maonesho ya vyuo yanayoendelea Jijini Arusha ambapo maonesho hayo yameandaliwa na NACT VET

Dkt kivuyo alisema kuwa Kwa kuwapeleka wanafunzi hao kwenye mahospitali hayo kunamuwezesha mwanafunzi kupata uzoefu wa kutosha

Alisema kuwa elimu hiyo mpaka sasa imeweza kuwasaidia Sana wanafunzi hao ambao wameweza kupata uzoefu ambao wanapata kuanzia shuleni mpaka kwenyw hospitali hizo za Jiji la Arusha

“Sisi tunajikita kutoa huduma Bora kwenye jamii kwa hiyo ni muhimu sana kuanza kuwaandaa wanafunzi hawa kwa ubora wa kimataifa ili baadae wawe chachu katika sekta hiyo ya afya”aliongeza Dkt kivuyo

Katika hatua nyingine alizitaja hospitali ambazo zimeweza kuwapa wanafunzi hao kipaumbele hasa katika kufanya mazoezi Kwa vitendo kuwa a ni pamoja na hospitali ya Mkoa wa Arusha Mt meru,hospitali ya levolosi,hospitali ya matenity Africa,hospitali ya Selian pamoja na hospitali ya Arusha Medical ambayo nayo inamilikiwa na kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania.

Awali aliwataka Vijana kuhakikisha kuwa wanatumia fursa ya chuo hicho ambacho kinapatikana Arusha kwa kuwa wameboresha huduma Kwa wanafunzi ili jamii nayo iweze kunufaika na utaalamu wa wataalamu kutoka katika chuo hicho