December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ally Kamwe ang’atuka Yanga

Afisa habari wa klabu ya Yanga Ally Kamwe ametangaza rasmi kuachia ngazi ndani ya klabu hiyo huku sababu kubwa ikitajwa ni kurejea kwa Haji Manara.

Ally Kamwe kupitia instagram yake ameandika: A Good dancer must know when to Leave a Stage, 𝑀𝑡𝑢𝑚𝑏𝑢𝑖𝑧𝑎𝑗𝑖 𝑚𝑧𝑢𝑟𝑖 𝑎𝑛𝑎𝑡𝑎𝑘𝑖𝑤𝑎 𝑘𝑢𝑗𝑢𝑎 𝑛𝑖 𝑤𝑎𝑘𝑎𝑡𝑖 𝑔𝑎𝑛𝑖 𝑤𝑎 𝑘𝑢𝑜𝑛𝑑𝑜𝑘a 𝐽𝑢𝑘𝑤𝑎𝑎𝑛𝑖.. 

Maneno ya hekima kutoka katika kinywa cha Patrick Loch Otieno Lumumba; Na ni Hekima hii, inanituma mbele yenu Wananchi, Mashabiki na Wanachama wa Klabu yetu pendwa, kuwaambia kuwa, Ni wakati sasa wa kijana wenu kuondoka Jukwaani.

Nimesimama Miaka miwili juu ya hili Jukwaa, Tumeimba, Tumecheza, Tumefurahi na Alhamdulillah Tumeshinda pamoja kila pambano Lililokuja mbele yetu.Muda wangu umemalizika na Asanteni sana. 

Tutaonana tena Wakati mwingine nikiwa na kitu kizuri cha kuwaonyesha Juu ya Jukwaa.

DaimaMbeleNyumaMwiko.

Mwenyekiti wa Wasemaji

Ally Kamwe.