BAADA ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Kamati ya Halmashauri Kuu ya CCM, Dkt John Pombe Magufuli, jana kutangaza majina ya wagombe wa Ubunge, Udiwani na Ubunge Viti Maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Wadau mbalimbali wa muziki baada ya kusikia baadhi ya wasanii wameteule akiwemo msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Mwana FA na Meneja wa Diamond Platnumz, Babutale wameonyesha furaha yao juu ya uteuzi huo.
” Nimefurahishwa sana kwani hii ni ishara kubwa kwa wasanii lakini pia kwa serikali kutambua mchango wa wasanii kwenye taifa hili,” wamesema.
Mwana FA ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa instragram kuwa “Mungu ni mwema sana, ni miongoni mwa zile siku chache, mimi nimeishiwa na sina la kusema, alama nyingine kuhusu ukubwa wa Mungu”.
More Stories
Mhandisi Mramba:Kuuza na kununua umeme ni jambo la kawaida kwa nchi
NCAA:Filamu za ‘Royal Tour’,Amaizing Tanzania zimechangia ongezeko la watalii Ngorongoro
NHIF yaeleza inavyotumia TEHAMA kudhibiti udanganyifu