December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ali Kiba aachia ngoma mpya ‘Salute’

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa lebo ya Kings music Alikiba, ameachia ngoma mpya ujulikanayo ‘Salute’ aliyemshirikisha msanii kutoka Nigeria Rudy boy, baada ya hivi karibuni kutamba na wimbo wake ‘Ndombolo’.

Akiweka wazi hilo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram amesema, aliwaahidi mashabiki wake kuwa anatoa vitu mfululizo mapaka album ya ‘Salute’ itimie kwa ajili ya kuwapa burudani Watanzania.

“Mashabiki wangu natimiza ahadi yangu.!! Nilisema nitoa nyimbo mfululizo mpaka Albamu itatupa * SALUTE * kwa kumshirikisha ndugu yangu Rudy boy. Hii ni Rekodi Maalum !! Furahiya wakati huu kumpongeza mpenzi wako,” amesema Ali Kiba.