Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka amewashukuru wadau mbali mbali ambao wanaendelea kujitokeza kusaidia wananchi walioathiriwa na mafuriko yaliyotokea katika siku za karibuni wilayani humo.
DC Shaka ameyasema hayo wakati akipokea msaada wa vitu mbalimbali kutoka kwa Ndugu Hidhi Abdallah Al Saedy kwa niaba ya kampuni ya AL- SAEDY ikiwemo magodoro zaidi ya 100, Unga wa Sembe mifuko 100, Sabuni ya kufulia na Maji ya kunywa.

Amesema Misaada hiyo inawapa faraja watu wote walipatwa na majanga hayo kwani wengi wao wamepoteza mali nyingi huku mashamba yao yakiharibiwa vibayaIkumbukwe kuwa hivi karibuni baadhi ya maeneo Wilaya ya Kilosa yalipitwa na changamoto ya mafuriko baada ya Mvua kubwa kunyesha katika mikoa ya Dodoma, Morogoro na Manyara kusabisha maafa makubwa kwa wananchi na mali zao.


More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi