Na Esther Macha, Mbeya
MWANAMKE mmoja aliyefahamika kwa jina la Joyce Akyoo ‘Manka'(31) mkazi wa Soweto na mfanyabiashara wa Jijini Mbeya anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani hapa kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo kuhusu ugonjwa wa corona kwenye mitandao ya kijamii.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoani hapa ,Ulrich Matei amesema kuwa, mtuhumiwa alikamatwa jana April 27 saa 7:30 mchana baada ya jeshi lhilo kufanya msako eneo la Stereo lililopo kata ya Manga Tarafa ya Sisimba.
Kamanda Matei amesema, Machi 30 mwaka huu saa 8.09 mchana mtuhumiwa huyo alituma taarifa za uongo na zenye lengo la kupotosha kuhusu ugonjwa wa Corona.
Kamanda Matei amesema, mtuhumiwa huyo alituma taarifa ugonjwa wa corona kwenye kundi “Fans of Mwailubi Car Wash” katika mtandao wa WhatsApp kwa kuweka picha za marobota ya nguo akieleza kwa maandishi kwa sauti baada ya kujirekodi mablangeti ya wagonjwa wa Corona ambao wamefariki nchini China na nguo hizo kuletwa Barani Afrika na ugonjwa Corona.
Mtuhumiwa huyo aliendelea kuongea na kuandika kuwa akitadhalisha watu wasikubali msaada huo hivyo tayari upelelezi wa shauri hilo unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria