March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ajinyakulia Mil. 5/- Kampeni ya Yas ‘tunasherehekea mwaka mmoja’

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

KAMPUNI ya Mawasiliano Yas, imekabidhi hundi ya shilingi milioni tano (5) kwa Lucy Mwaikena, mkazi wa Bunda mkoani Mara, aliyeshinda katika droo ya kila wiki ya Kampeni ya “Tunasheherekea Pamoja – Mwaka Mmoja wa Yas.”

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo, Meneja wa Yas Kanda ya Mara Kusini, Halid Mtwange amesema kampeni hiyo imebuniwa mahususi kuwazawadia wateja wanaotumia huduma za Yas kwa kuwakabidhi zawadi za kila siku, kila wiki na kila mwezi.

Amesisitiza kuwa, wateja wanaoendelea kununua vifurushi vya Yas huongeza nafasi zao ya kujishindia zawadi hizo.

Aidha, amesema kampeni hiyo imeandaliwa mahsusi kwa ajili ya kuwashukuru wateja na kuwataka wakazi wa Bunda kuchangamkia fursa zinazotolewa na Yas ili kujishindia zawadi mbalimbali.

Amebainisha kuwa, Kampeni hiyo inatoa motisha ya ushindi kupitia zawadi za kila siku, kila wiki na kila mwezi, na kwamba kadri mteja anavyotumia vifurushi vya Yas ndivyo anavyoongeza nafasi yake ya ushindi.

Kwa upande wa mshindi, Lucy Mwaikena ameishukuru Yas kwa kukamilisha ahadi ya ushindi wake na kwamba fedha hizo zitamsaidia kwenye mambo mbalimbali ikiwemo Ada za watoto na kukamilisha Ujenzi wa nyumba.

Kampeni ya ‘Tunasheherekea Pamoja – Mwaka Mmoja wa Yas’ inaendelea kote nchini, na wateja wanaendelea kupata nafasi ya kuingia kwenye droo kupitia matumizi yao ya kawaida ya huduma za mawasiliano za Yas.

Zawadi ya shilingi milioni 100 ya mwisho wa Kampeni ipo mbioni kutolewa na watanzania wametakiwa kuchangamkia fursa hiyo