Na Rose Itono,Timesmajira
KAMPUNI ya Airtel Tanzania imezindua maduka mengine manne ya kisasa ili kuwapunguzia adha wananchi kutumia gharama kufuata huduma
Akizungumza kwenye uzinduzi huo leo Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma kwa wateja wa Kampuni hiyo Adriana Lyamba amesema uzinduzi wa maduka hayo utawapunguzia adha wananchi kufuata huduma mbali na maeneo wanayoishi
Amesema maduka hayo ambayo ni ya kisasa yatawezesha wateja wanaotumia mtandao wa Airtel kupata huduma bora na za kisasa
“Leo tumezindua tena maduka manne Jijini Dar es Salaam na kufanya Dar es Salaam kuwa na Jumla ya maduka kumi ambayo yatatoa huduma bora na za kisasa,” amesema Liamba na kuongeza kuwataka wananchi kijivunia maduka hayo kwa kupata huduma bora

Kwa upande wake Msimamizi Mkuu wa maduka hayo kutoka Airtel Gaspa Ngowi ameyataja maeneo ambayo yamefunguliwa maduka hayo Leo kuwa ni Kawe,Sinza,Mikocheni na Mwananyamala
Amesema wananchi wa maeneo hayo wataweza kupata huduma zote kama zinazopatikana Makao Makuu ya Airtel ikiwa ni pamoja na kusajili laini, kupata simu za mkopo sambamba na vifurushi Vya intaneti
Amezitaja huduma zingine kuwa ni pamoja na kujisajili na kubadili laini za simu
Huduma za Airtel Money kwa wateja na mawakala,
Mauzo ya vifaa vya Home Broadband kwa ajili ya intaneti majumbani ikiwemo router za 5G na MiFi kubadilisha nywila ya Airtel Money na kurejesha akaunti
Mauzo ya simu janja na vifaa vingine

Ameongeza kuwataka wananchi kutumia fursa hiyo kwa kupata huduma karibu ili kupunguza gharama za kufuata huduma mbali
Hata hivyo amesema maduka haya ya kisasa ni moja ya ahadi ya Airtel kujali wateja wake Tanzania nzima na kuwapa huduma iliyobora na ya kiwango cha juu popote pale
More Stories
Mkurugenzi Lazaro Twange wa TANESCO atua TGDC
Rais wa Finland afurahishwa na uhifadhi wa historia nchini
Sekta ya madini yakusanya zaidi ya bil.900 hadi kufikia Mei 15,2025