Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Airtel Tanzania imezindua rasmi teknolojia mpya ya Voice over LTE (Airtel VoLTE), hatua ambayo inaendelea kuonesha dhamira ya Airtel ya kuendelea kutoa huduma za mawasiliano ya kisesa yaani BILA CHENGA kwa wateja wake nchini kote.
Kupitia teknolojia ya Airtel VoLTE, wateja wa Airtel walio na simu janja zenye uwezo wa 4G na 5G wataweza kupiga na kupokea simu kupitia mtandao wa 4G na 5G kwa ubora wa juu na kasi zaidi, huku wakifurahia mawasiliano bora kama wako katika mazungumzo ya ana kwa ana yaani BILA CHENGA.
Tekinolojia ya Airtel VoLTE inawapa wateja uwezo wa kupiga simu huku wakiendelea kutumia intaneti bila usumbufu, jambo linaloongeza ufanisi wa huduma za kidijitali.
Mbali na ubora wa sauti, teknolojia Airtel VoLTE pia inachangia kuokoa matumizi ya betri ya simu yako na kuifanya idumu zaidi na kutoisha haraka, kuongeza kasi ya kuunganisha simu na kuruhusu wateja kubadilika kutoka simu ya sauti kwa urahisi BILA CHENGA na pia bila gharama ya ziada. Mara tu huduma inapowashwa katika kifaa au simu yako yenye uwezo wa Airtel VoLTE, mteja huanza kufurahia huduma hiyo moja kwa moja bila kuhitaji usajili.
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Charles Kamoto, amesema kuwa kuanzishwa kwa Airtel VoLTE – BILA CHENGA ni hatua muhimu iliyopo ndani ya dhamira ya Airtel katika kuhakikisha watanzania wanaendelea kupata huduma bora na za kisasa.

“Uzinduzi huu ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kuendeleza uwekezaji mkubwa na ubunifu ili kuhakikisha mawasiliano yanapatikana kwa kasi, ubora na uhakika—kwa kifupi, mawasiliano BILA CHENGA,” amesema Kamoto.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uhandisi wa Mtandao wa Airtel Tanzania, Prosper Mafole amesisitiza kuwa Airtel inaendeleza kuboresha na kusambaza miundombinu ya kisasa ya mawasiliano ili kuzidi kuboresha maisha ya mteja wa kawaida, wa kibiashara na wa taasisi.
Ameeleza kuwa Airtel VoLTE inaleta kiwango kipya cha ubora katika mawasiliano ya simu na ni sehemu ya mkakati mpana wa Airtel kuchangia kutimiza agenda ya serikali ya Tanzania ya kidijitali kutokana na kasi na ufanisi— Call- BILA CHENGA.

Uzinduzi wa teknolojia hii unaimarisha zaidi dhamira ya Airtel Tanzania ya kukuza ujumuishaji wa kidijitali, kuongeza ubora wa huduma na kuhakikisha kuwa kila mteja, awe nyumbani, kazini au kwenye shughuli za biashara, anapata uzoefu wa mawasiliano ulio imara, wa kisasa BILA CHENGA.
Miongoni mwa vipengele muhimu katika teknolojia hiyo ni pamoja na mawasiliano ya simu ya kiwango cha juu,mazungumzo yanasikika vizuri mithili ya watu wanaozungumza ana kwa ana,
Kuunganisha Simu kwa Haraka na Simu huunganika kwa kasi mara tatu zaidi ya mitandao ya kawaida.

More Stories
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI