KAMPUNI ya Mawasiliano ya Mtandao wa Airtel imewaomba wateja na mawakala wanaotumia mtandao huo kuendelea kuchangamkia promosheni maalum ya Airtel Santa Mizawadi ili waweze kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu.
Akizugumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam mapema leo Desemba 20,2024 Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano, Jackson Mmbando amesema promesheni hiyo bado inaendelea na droo ya kwanza itafanyika Jumanne Disemba 24 mwaka huu
Amesema Airtel Santa Mizawadi ni promosheni kabambe ambayo itawapa washindi fursa ya kuondoka na zawadi kemkem ikiwemo pocket WiFi, simu janja, pikipiki, runinga na pesa Taslim hadi shilingi milioni moja.
“Jinsi ya kushiriki na kujishindia Mizawadi ya Airtel Santa Mizawadi, Wakala wa Airtel atatakiwa kufanya miamala ya kuweka na kutoa fedha, ambapo pia ili Mteja aweze kuingia kwenye droo anatakiwa tu kufanya miamala kama vile kununua bando, Kutuma pesa, kutoa pesa, kulipa bili, kufanya miamala ya kibenki, kutuma au kupokea pesa nje ya nchi, kununua muda wa maongezi.
Kwa upande Meneja wa huduma kwa wateja, Celine Njuju amesema mtandao wa Airtel umekuwa ukiwathamini sana wateja wake pamoja na mawakala ndo maana wameamua kuja na Airtel Santa Mizawadi katika msimu huu wa sikukuu
Amesema katika msimu huu balozi wa mtandao huo Mr Santa atakuwa akizunguka katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kutoa zawadi mbalimbali na kemkem kwa mawakala
“Ndugu mteja , Wakala usipitwe na zawadi hizi kutoka kwa Mr Santa..”amesema
Vilevile amesema droo ya kuwapata washindi itakuwa ikifanyika mara moja kwa wiki siku ya Jumanne na kusisitiza kuwa washindi watakuwa wakipigiwa simu kupitia namba 100 pekee na kuambiwa ni kitu gani ameshinda katika droo hiyo.
“Mteja wetu usikose kuendelea kutumia huduma zetu za Airtel ikiwemo kuweka Pesa na kutoa, kulipa bili mbalimbali ili kuweza kuingia katika droo ya kujishindia zawadi mbalimbali.
Naye msanii maarufu Lucas Lazaro maarufu (Joti) ambaye ni Mr. Santa amesema kuwa msimu huu wa sikukuu Airtel inawajali wateja wake kwa kutoa zawadi Kem Kem kwa kufanya miamala mbalimbali kwa kulipia bili, kutuma na kupokea pesa, nunua cho chote ambapo unajitengenezea nafasi kubwa ya kupata zawadi.
More Stories
Wakazi 359,577 Kaliua wapata maji safi
Bil. 19 za Benki ya Dunia kuing’arisha Manispaa Tabora
Halmashauri zatakiwa kuchechemua fursa za biashara mpakani