Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
Airtel Tanzania imezindua rasmimaduka matano mapya ya Airtel Smart Shop jijini Mwanza, hatua inayolenga kupanua huduma za kidijitali na kuimarishaujumuishaji wa kifedha katika Kanda ya Ziwa.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Saidi Mohamed Mtanda, ameieleza kuwa Mwanza nikitovu muhimu cha uchumi katika ukanda huo, ukiwa nashughuli kuu za uvuvi katika Lake Victoria, biashara ndogo naza kati, kilimo cha pamba na mazao ya chakula, uchimbajimadini pamoja na huduma na utalii.
“Mawasiliano ya kuaminika ni muhimu kwa wavuvi katika ZiwaVictoria ili kuratibu mauzo na malipo kidijitali. Vivyo hivyo, kwa wafanyabiashara katika masoko makubwa kama Soko Kuula Mwanza na Kariakoo, Airtel Money hurahisisha miamala, ukusanyaji wa malipo na uagizaji wa bidhaa.
Kwa wakulima wapamba na mpunga, muunganisho wa kidijitali unawaunganishana masoko na taasisi za kifedha, Uwekezaji wa Airtel unaungamkono moja kwa moja shughuli hizi muhimu za kiuchumi,” pia ameiipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya RaisSamia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwekeza katika uchumiwa kidijitali na miundombinu ya TEHAMA.
“Serikali imeweka mazingira wezeshi yanayochochea uwekezajikatika sekta ya mawasiliano, jambo linalosaidia kuongeza fursaza kiuchumi na kuboresha maisha ya wananchi,” ameongeza.
Kwa mujibu wa takwimu za robo ya nne ya mwaka 2025 za Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA), usajili wa laini za simu umeongezeka kutoka milioni 99.3 hadimilioni 106.9, usajili wa intaneti umeongezeka kwa asilimia 3.2, huku matumizi ya intaneti kwa simu yakiongezeka kwa asilimia9.5. Upenyaji wa simu janja umefikia asilimia 41.82 naupatikanaji wa mtandao wa simu kwa ujumla kufikia asilimia87.11.
“Takwimu hizi zinaonyesha kuwa mawasiliano ni kichocheokikuu cha maendeleo ya kijamii na kiuchumi, yakirahisishabiashara, kuvutia uwekezaji na kuongeza kipato cha mtu binafsina taifa kwa ujumla,” amesema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja waAirtel Tanzania, Adriana Lyamba, amesema maduka hayo mapyayamebuniwa kwa mfumo wa kidijitali usiotumia makaratasi, yakiwa rafiki kwa wateja na jumuishi, ikiwemo kuwazingatiawatu wenye ulemavu.
“Kila duka lina uwezo wa kuhudumia zaidi ya wajasiriamali nabiashara ndogo 400, kwa kuwapatia huduma za haraka, sahihi nazenye ufanisi katika masuala ya kidijitali na kifedha,” amesema.
Naye Meneja wa Airtel Business Kanda ya Ziwa, Malaki Macha, amebainisha mchango wa uwekezaji huo kwa uchumi wamkoa huo.
“Kupitia Smart Shops hizi mpya, tunaendelea kuunga mkonosekta muhimu za uchumi wa Mwanza, zikiwemo uvuvi, biashara, kilimo na huduma mbalimbali kwa kutoa suluhisho za mawasiliano ya kuaminika na malipo ya kidijitali,”
Kwa mujibu wa kampuni hiyo, Mkoa wa Mwanza una zaidi yawateja milioni 1.2 wa Airtel, wanaohudumiwa na zaidi yamawakala 15,000 wa Airtel Money pamoja na minara yamawasiliano inayohakikisha upatikanaji wa mtandao hata katikamaeneo ya pembezoni.
Uzinduzi wa maduka hayo matano mapya unaelezwa kuwa nisehemu ya mkakati wa Airtel Tanzania wa kuimarisha hudumabora za kidijitali, kuchochea ukuaji wa uchumi, kuongeza ajirakwa vijana na kuunga mkono ajenda ya taifa ya uchumi wakisasa unaotegemea teknolojia.

More Stories
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina
Kihongosi: Msigombane kwa itikadi za vyama