June 16, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Airtel Tanzania yaungana na Infinix kuzindua NOTE 50 Pro+

Na Rose Itono,Timesmajira

Airtel Tanzania, kwa kushirikiana na Infinix Tanzania imezindua simu mpya ya Infinix NOTE 50 Pro+, ili kuimarisha upatikanaji na uwezo mzuri wa simu za mkonon nchini

Akizungumza kwenye uzinduzi huo Dar es Salaam Mtaalamu wa Bidhaa wa Infinix Tanzania, Lilian Julius, amesema Infinix NOTE
50 Pro+ ni simu ya kisasa inayoendana na maisha ya Teknolojia ya kisasa

Amesema simu hiyo inapatikana kwenye maduka yote ya Airtel yaliyoko nchini ambapo Kampuni zote mbili zilizoungana kuzindua
zinatumia teknolojia ya hali ya juu na ya kutegemewa na watanzania wengi.

“Kifaa hiki ni mchanganyiko kamili wa ubunifu na umaridadi, na baadhi ya vipengele vinavyoifanya kuwa bora zaidi ni pamoja na kipengele kinachoendeshwa na teknolojia ya Akili Mnemba (AI), ” amesema Julius na kiongeza Ushirikiano wetu na Airtel Tanzania unakusudia kuimarisha upatikanaji na uwezo mzuri simu ya mkononi nchini Tanzania.

Kwa upande wake, Meneja wa Vifaa vya Intaneti wa Airtel Tanzania, Asnath Mboya, amesema kuwa Infinix NOTE 50 Pro+ ni tumaini jipya ambalo limedhamiriwa kukidhi mahitaji ya wateja wa Airtel kote Tanzania kwa kuwa linatoa kasi na thamani isiyo na kifani, na kuongeza kuwa ushirikiano huo unakamilisha juhudi endelevu za Airtel Tanzania za kukuza uhusiano na wadau mbalimbali kwenye tasnia ya teknolojia na ubunifu ili kukuza uwezo wa kutumia simu za mkononi na kuongeza tija.

Ameongeza kuwa pamoja na uzinduzi wa kifaa hiki cha kubadilisha ushindani kwenye soko la simu za mkononi, tunasaidia kuboresha maisha ya kidijitali kwa wateja wetu kwa kuwawezesha kuwa na simu mahiri ambayo inabadilisha jinsi wanavyowasiliana, kufanya kazi na kufurahia ulimwengu wa kidijitali.

“Hatua hii inaendana na dhamira yetu ya kuona watanzania wote wanapata huduma za simu za kidijitali kwa bei nafuu, hivyo kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijitali,” amefafanua Mboya

Mboya amesema elez
lengo la uzinduzi huu ni kuwapa vijana na wapenzi wa teknolojia kifaa kinachochanganya ufanisi, akili na mtindo wa kisasa. Kufanya kazi pamoja na Infinix kunahakikisha kwamba simu hii inapatikana kwa mamilioni ya watu kote nchini.”

Amezitaja baadhi ya vivutio muhimu vya NOTE 50 Pro+ kuwa ni pamoja na: kuwa na
Betri ya 5200mAh yenye uwezo wa kuchaji haraka wa 3.0, ikichajiwai kamili kwa dakika 38 pekee.
Uzoefu wa hali ya juu wa One-Tap AI unaoendeshwa kwa usaidizi wa mfumo wa Akili Mnemba uitwao ‘Folax AI’ kwa ajili ya kutafsiri bila data, utambuzi wa maudhui na usaidizi wa wakati halisi.

Vingine ni Kamera ya 100X Periscope na lenzi ya mbele ya 50MP pamoja na sensa ya SONY IMX896 kwa upigaji picha wa hali ya juu, hata nyakati za usiku.

Amesema ushirikiano huu wa kimkakati ni ishara tosha ya maono ya pamoja kati ya Airtel na Infinix, kuwawezesha Watanzania kwenye teknolojia inayorahisisha, kuinua na kutajirisha maisha ya kila siku.