Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Airtel Tanzania kwa kushirikiana na TECNO, wameandaa droo ya mwisho ya Airtel Upige Mwingi Mpaka AFCON, ambayo imewapa nafasi wateja wa Airtel kujishindia zawadi kabambe zikiwemo pikipiki, friji, televisheni za kisasa Pamoja na simu janja za TECNO Spark20..
Akizungumzia na waandishi wa habari, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando, ametoa shukrani za dhati kwa wateja wa Airtel waliotumia huduma kwa kipindi chote cha promosheni ya Airtel Upige Mwingi Mpaka AFCON ilivyosaidia kukuza ushiriki wa jamii na kutangaza utalii wa Tanzania kupitia michezo.
“Tunapenda kuwashukuru wateja wote wa Airtel kwa ushiriki wao wa kujitolea katika promosheni hii. Airtel Upige Mwingi Mpaka AFCON imedhihirisha Airtel Tanzania ndiyo kampuni kubwa ya mawasiliano ambayo inathamini wateja wake kupitia huduma na bidhaa tunazotoa. Kupitia promosheni ya Airtel Upige Mwingi Mpaka AFCON, wateja wote wa Airtel walipata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali ambazo zinaenda kuacha alama katika maisha yao kibiashara na ndani ya ulimwengu huu wa kidigitali,” amesisitiza Mmbando.
Mmbando ameendelea kusema kuwa “Februari 10 mwaka huu, Airtel Tanzania na TECNO iliwadhamini Marcel Leonard, Jafari Salukele, Alfred Mlita na John Kimario kwenda kutazama fainali za AFCON moja kwa moja nchini Ivory Coast. Kupitia safari ile, watabaki na kumbukumbu na wataendlea kuzienzi waliojifunza nje ya nchi.
Nickson Mollel, Mmoja wa washindi wa promosheni hiyo ametoa shukrani kwa Airtel Tanzania huku akieleza kuwa zawadi yake pikipiki aliyoshinda sasa inamwezesha kufungua biashara ya bodaboda ambayo sasa anaisimamia.
“Promosheni ya Airtel Upige Mwingi ilinibariki kwa pikipiki iliyonifanya nianzishe biashara. Sikuitarajia zawadi hii lakini kwa sasa hivi inanisaidia kupata riziki. Nawahimiza wateja wengine wa Airtel kushiriki katika promosheni za Airtel siku zijazo,” amesema.
Kampeni ya Airtel Upige Mwingi ilianza rasmi Januari 8, mwaka huu ikiwa na lengo la kuwazawadia wateja wa Airtel Pamoja na kuwawezesha kushiriki katika utalii na michezo wakati wa msimu wa mashindano ya AFCON yaliliyofanyika kule Ivory Coast..
Ndani ya miezi mitatu ya promosheni ya Airtel Upige Mwingi Mpaka AFCON, wateja wa Airtel walipewa fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo muda wa maongezi, bando, pikipiki, friji, televisheni za kisasa na simu janja za TECNO spark 20.
Zawadi hizo za Airtel Upige Mwingi zinalenga kurudisha kwa wateja pamoja na kuchochea matumizi ya huduma bora za kidijitali kutoka Airtel.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi