June 14, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Airtel Tanzania NEMC wafanya usafi ‘Beach Kidimbwi’ kutokomeza taka za plastiki

Na Rose Itono,Timesmajira

Airtel Tanzania Leo Juni 13 imeungama na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ( NEMC) kufanya usafi kwenye fukwe ya Bahari ya Kidimbwi maarufu Beach Kidimbwi’ iliyopo Kata ya Kawe Mtaa wa Mbezi Beacha B Dar es Salaam ili kutokomeza taka za plastiki

Pia Airtel imekabidhi vifaa Vya usafi kwa Uongozi wa Mtaa wa Mbezi Beach B ili kuendeleza usafi na kufanya mazingira yabaki salama

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mara baada ya zoezi la usafi kumalizika Kaimu Meneja wa Mazingira Kanda Ya Mashariki Kaskazini

Beatrice Singano amesema huu ni muendelezo wa siku ya Mazingira Duniani ambayo kilele chake kulikuwa ni Juni 5 mwaka huu

Pia Airtel inaungana na serikali katika mkakati wake wa kuweka.mazingira safi na kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki kwa Kauli mbiu ya Pamoja tutokomeze taka za plastiki

” Leo tumeungana na NEMC, Halmashauri ya Kinondoni,viongozi wa Mtaa wa Mbezi Beach B na wananchi wake kufanya usafi ufukwe wa Kidimbwi maarufu ‘ Beach Kidimbwi’ ili kutokomeza taka za plastiki ambazo zinachangia kuharibu mazingira na kuzuru viumbe wa bahari,” amesema Singano

Aidha amewataka wananchi kubadili tabia na kupunguza taka za plastiki ili kulinda viumbe wa bahari ambao wanachangia ukuaji wa uchumi wa nchi

Amesema Airtel itaangalia namna ya kuweka utaratibu wa kudumu kuhakikisha wanajipanga kufanya usafi kwenye fukwe ili ziweze kubaki salama

Kwa upande wake Afisa Mazingira Mwandamizi akimwakilisha Kaimu Meneja wa Mazingira Kanda Ya Mashariki Kaskazini Jeremia Nyakwaka amewataka watanzania kulinda na kuhifadhi mazingira ya fukwe ili yaweze kubaki salama

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbezi Beach B Asha Vionatis ameishukuru Airtel kuungana na wananchi wa mtaa wake kufanya usafi kwenye fukwe hiyo na kuomba zoezi hili liwe endelevu ili kulinda Mazingira ya fukwe sambamba na kuyaweka yabaki salama kwa viumbe Vya makini na jamii pia

Hata hivyo ameshukuru kwa vifaa vilivyotolewa kwa ajili ya kuendeleza usafi katika Mtaa huo huku akiahidi kushirikiana na wananchi wake kuhakikisha fukwe na.mtaa wao kwa ujumla.unakuwa wa kuigwa kwa suala la usafi