May 18, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Airtel Afrika yateua Publics Groupe Africa kuwa mbia wake katika masoko 12 Barani Afrika

Na Rose Itono,Timesmajira

Airtel Afrika imeiteua rasmi Publicis Groupe Africa kuwa mshirika wake wa masoko 12 Barani Afrika

Taarifa iliyotolewa na Kitengo Cha Mawasiliano na Masoko Cha Airtel Tanzania imesema kuwa baada ya mchakato mpana wa uwasilishaji wa mapendekezo ya ubia uliofanyika Johannesburg Airtel Africa
imeiteua rasmi Publicis Groupe Africa kuwa mshirika wake wa masoko ya pamoja katika masoko 12 muhimu barani Afrika, ikiwa ni pamoja na Tanzania.

“Ushirikiano huu wa kimkakati unaashiria hatua kubwa katika maendeleo ya masoko barani Afrika, ukileta pamoja taasisi mbili zenye nguvu na maono ya pamoja ya kutoa huduma za kibunifu zinazotegemea data, zenye mvuto kwa hadhira mbalimbali za bara hili,” inasema taarifa hiyo

Taarifa unazitaja nchi zitakazokuwepo kwenye ushirikiano huu kuwa ni pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo DRC, Congo Brazzaville,
Niger, Chad, Gabon, Kenya, Uganda, Rwanda, Tanzania, Zambia, Malawi na Madagascar, na kwamba majadiliano kuhusu masoko mengine bado yanaendelea

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Publicis Groupe Africa Koo Govender anasema Airtel Africa, ni kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma za mawasiliano na kifedha, inayofanya kazi kwa malengo mahususi ya kubadilisha maisha ya watu kwa kuwaunganisha wale wasiokuwa na mawasiliano, kuwafikia watu wenye uhaba wa huduma za kifedha na pia kuziba ufa wa kidijitali katika maeneo inapotekeleza operesheni zake.

Anasema kujidhatiti kwakampuni hiyo katika uvumbuzi, ujumuishaji na upatikanaji wa huduma ndio umeifanya iwe ni chapa yenye matokeo makubwa.

“Ushirikiano huu si tu kielelezo cha ushindi kwa Publicis Groupe Africa, bali pia ni ushuhuda wa aina mpya ya masoko bila mipaka ya ushirikiano wa kweli na wa kuangalia mbele kwa mustakabali wa Afrika,” anasema Govender

Anaongeza tunathamini sana imani ambayo Airtel imetupa na tunatazamia kushirikiana kwa karibu katika kujenga chapa yenye athari kubwa na ya maana kwa bara letu

Anasema Publicis Groupe Africa, kupitia tawi lake la The Partnership Africa lililopo Nairobi, liliwasilisha mkakati bora unaojumuisha mbinu za kibunifu, hadithi zenye mvuto, usimamizi wa vyombo vya habari, suluhisho za kidijitali na matumizi ya data ili kuunga mkono malengo ya muda mrefu ya Airtel.

Hata hivyo kupitia mtandao wake wa washirika barani Afrika, ushirikiano huu utawezesha utekelezaji wa kampeni muhimu kwa uwanda mpana kwenye kila soko, pamoja na kutunza tofauti za kitamaduni.