Na Allan Vicent, TimesMajira Online, Tabora
KIJANA wa miaka (19) Juma Mussa Mkazi wa mtaa wa Uzunguni kata ya Malolo katika Manispaa ya Tabora amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumlawiti mtoto wa kiume wa miaka mitano (5) .
Akitoa hujumu hiyo Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Tabora John Mdoe alisema ametoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa wananchi wengine wenye tabia kama hizo.
Awali Wakili wa Serikali Jaines Kiwelo aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Januari 26, 2022.
Katika ushahidi wake mhanga wa tukio hilo aliiambia mahakama kuwa siku hiyo aliitwa na mtuhumiwa (Juma Mussa) kisha akamwambia avue nguo ndipo alianza kumlawiti kwa kumfunga mdomo asipige kelele.
Wakili Kiwelo aliiambia Mahakama kuwa mshitakiwa mara baada ya kufanya unyama huo alimpa sh 200 akamnunulie sigara moja na chenji iliyobaki sh 100 akamwambie akanunue Jojo.
Mama Mlezi katika ushahidi wake aliiambia Mahakama kwamba aligundua mtoto huyo kulawitiwa kutokana na kutoa harufu ya kinyesi na kwamba hata kutembea alikuwa anachechemea.
Baada ya kumwona mtoto wake akiwa kwenye hali hiyo alimpekua na kumkuta akiwa ameharibiwa vibaya sehemu zake za haja kubwa.
Aliongeza kuwa alipomwuliza mwanae akasema amemfanyiwa ukatili huo na Juma ambaye alimwita chumbani kwake na kuanza kumfanyia unyama huo.
Dkt aliyemfanyia vipimo mtoto huyo katika ushahidi wake aliiambia mahakama kuwa aliimkuta sehemu ya haja kubwa ikiwa wazi akiwa ameumizwa vibaya .
Katika utetezi wake ili apunguziwe adhabu mshitakiwa alikana kufanya tukio hilo huku akidai kuwa anasingiziwa kutokana na ugomvi wa ujirani.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini