Gauteng, Afrika Kusini
MAOFISA wa afya katika Jimbo la Gauteng nchini Afrika Kusini ambako ndiko kunaongoza kwa maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona, wamesema kuwa mamlaka za nchi hiyo zinaandaa maeneo yenye makaburi 1,500,000 wakati visa vya janga hilo ambavyo vimedhibitishwa vinaendelea kuongezeka.
Bandile Masuku, daktari mwandamizi ambaye ni mjumbe wa baraza la utendaji jimboni humo, amekaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa ilikuwa ni jukumu la umma kuhakikisha kutokuwepo kwa makaburi hayo.
“Ni majadiliano ambayo wanajamii wanajisikia vibaya,” alinukuliwa akisema.
Jimbo la Gauteng linajumuisha majiji ya Johannesburg na Mji Mkuu wa nchi hiyo, Pretoria. Idadi ya matukio yanayohusu virusi vya Corona jijini humo sasa inazidi 71,000, ama asilimia 33 ya visa vyote Afrika Kusini.
Nchi hiyo ina zaidi ya visa 215,000 vilivyothibitishwa, na inatuma baadhi ya taarifa zenye idadi kubwa zaidi duniani za visa vipya vilivyoripotiwa.
Wakati huo huo, ulegezaji hatua za kudhibiti covid-19 maarufu ‘lockdowns’ nchini humo unaendelea.
More Stories
Dk. Mpango amwakilisha Samia sherehe za Uhuru wa Lesotho
Samia atangaza Tanzania kumuunga mkono Odinga
Tanzania yaongoza kikao maalum cha nishati safi