March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

African Quality Spices waja na ofa ya rejareja maonesho ya sabasaba

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online

WAUZAJI na wasambazaji wa bidhaa za Kilimo kutoka kampuni ya African Quality Spices ltd ( AQS), wamewaomba wananchi kutoka ndani na nje ya nchi, kuendelea kutumia bidhaa zao, wakidai kuwa zimethibitishwa kwa ubora wa hali ya juu.

Akizungumza kwenye maonesho ya kimataifa ya 49 ya Sabasaba yanayoendelea kufanyika Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo inayojihusisha na usambazaji wa bidhaa mbalimbali zinazotokana na Kilimo ikiwemo nyama na asali, Mussa Ngariba amesema, kampuni hiyo imeanza kufanya kazi ya kusambaza na kuuza bidhaa zake nje ya nchi kwa kipindi Cha muda mrefu huku wakipata matokeo chanya kutoka kwa walaji hao.

“Sisi kama wauzaji na wasambazaji wa bidhaa za Kilimo kutoka katika kampuni hii yetu, tunajivunia sana kupata matokeo mazuri kutoka kwa wateja wetu hususani nje ya nchi kwani ndiyo wateja wetu wakubwa, hivyo tunaendelea kuwaomba watanzania na raia wa kigeni kuendelea kuziamini bidhaa zetu kwani kila siku tunaendelea kuboresha huduma zetu” amesema Ngariba.

Aidha akizungumzia ushiriki wa Kampuni hiyo kwenye maonesho ya sabasaba amesema kuwa, wanaishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha maingira kila mwaka katika maonesho ya sabasaba, huku akiwasisitizia wananchi wote wanaofika katika maonesho hayo kupiga katika banda la African Quality Spices, ili kujionea bidhaa zao na kuweza kununua kwa rejareja tofauti na siku nyingine ambazo huuzwa kwa jumla.

” Tunaomba wananchi wote wanaofika katika maonesho hapa sabasaba waweze kupita katika banda letu ili wajionee bidhaa zetu nzuri na zenye ubora, lakini pia hapa watapata fursa ya kununua kwa rejareja tofauti na siku nyingine kwani huwa tunauza kwa jumla tu”, ameongeza Ngariba.