Na MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya Usafirishaji wa Anga ya Ufaransa KLM (AFKLM) ina mpango wa kuongeza kiwango cha wasafiri katika nusu ya pili ya mwaka 2023 sawa na asilimia 88 ya kiwango cha mwaka 2019.
Kutokana na kuwa na ongezeko la wageni, kampuni hiyo ilifanya tathmini ya kiwango cha ukuaji wa mapato kwa asilimia 88 ikiwa ni trilioni 1.64 ambayo ni ongezeko la bilioni 869.59 ya mwaka 2022.
Kampuni hiyo inakadiria kuongeza usafirishaji kwa kiwango kikubwa zaidi kutoka mwaka 2019 hadi 2024.
Hiyo inatokana na kuongezeka kwa kiwango cha wasafiri katika nusu ya pili ya mwaka 2023 kwa asilimia 8.2 au milioni 24.7 za wasafiri kupitia safari zake ikilinganishwa na tathmini ya kipindi cha Juni cha mwaka 2022 ikiwa ni ongezeko la asilimia 88 ya kiwango cha mwaka 2019.
Kutokana na matokeo hayo, kiwango cha nusu ya mwaka kilichoongezeka kutoka asilimia 8.2 hadi kufikia asilimia 11.6, kiwango cha mizigo kiliongezeka kwa pointi 2.6 kulinganisha na mwaka jana hivyo kusababisha safari katika shirika hilo kuongezeka zaidi.
Akizungumza wakati wa kutoa matarajio ya mwaka 2024, Meneja Mkuu wa AFKLM Mashariki na Kusini mwa Afrika, Nigeria na Ghana, Marius Van der Ham anasema wanafurahi kuona shirika lao limeinuka tena baada ya kuwa kimya kwa muda kutokana na changamoto ya COVID 19.
Ambapo mikakati yao ni kuongeza ubunifu na kuinua tena safari zao ikiwemo kuwekeza katika teknolojia, ubora wa ukaribishaji wa wageni na usafiri bora wa anga.
“Tuna ujasiri kusema kwa maboresho hayo mwaka 2024 siyo tu tutafikia kiwango cha mwaka 2019, bali kuhakikisha tunaweka mipango mizuri ya kisasa inayoendana na soko,ongezeko hili la wasafiri na mizigo linatokana na ubora wa mipango yetu, kazi kubwa na nzuri inayofanywa na timu yetu ikiwemo kuongeza imani kwa wasafiri wetu,”.
Katika kipindi cha robo ya tatu na ya nne ya mwaka 2023, shirika linatarajia kufanya usafirishaji kwa asilimia 95 ikiwa ni sawa na kiwango cha kilometa milioni 128.26 zilizosajiliwa mwaka 2022.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu