Na Mary Margwe, TimesMajira Online, Ruangwa
Afisa Ushirika wa Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi Patroba James Andele amewataka wananchi kuchangamkia fursa ya Maonyesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji 2023 yanayoendelea Wilayani Ruangwa kwa kuanzisha vyama vya Ushirika wa madini.
Hayo alibainisha jana wakati alipokua akizungumza na baadhi ya Wananchi waliokwenda kutembelea Banda lao la Maonyesho la Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania ( TCDC) kwenye Maonyesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji 2023 yaliyofanyika katika Viwanja vya Soko Jipya Wilayani Ruangwa.
Andele amesema Ushirika wa madinii utawawezesha kukopesheka kiurahisi kwenye mabenki na kadhalika kupata masoko ya kuudhia Madini kiurahisi pia, hivyo amewataka wananchi kuchangamkia hiyo fulsa ya uanzishwaji wa ushirika wa Madini.
“Tupo hapa kuhamasisha wananchi kuanzisha ushirika wa Madini, ambapo utaratibu wake unajulikana wa kuwa na Watu wasiopungua 10 au zaidi ya 10, ambapo viko vyama vingi vya ushirika kama ushirika wa mazao ya ufuta, korosho na mengine, ushirika wa Madini utaweza kupata maeneo makubwa ya kuchikba madini” amesema Andele.
Aidha alifafanua kuwa Ushirika ni Kikundi au jamii ya watu wanaokubaliana kwa hiari yao wenyewe kuanzisha Chama Cha ushirika kwa lengo la kuinuana kiuchumi na kuweza kukabiliana na ushindani wa Soko.
Kwa upande wake Anuary MwinyiMkuu ambaye ni Mtunza ghala la vifaa vya chama kikuu cha ushirika Lindi Mwanbao Coop union ambacho kinahudumia Halmashauri tatu, Kilwa, Mtama na Lindi Manispaa amempongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuutendea haki Ushirika, ambapo kwa sasa pembejeo zimefika hadi Vijijini huku watu wakigawana pembejeo kutokana na Ushirika huo.
MwinyiMkuu amesema Rais Samia katika uongozi wake amefanya mambo makubwa na ya mfano unapaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania kutokana na juhudi kubwa anazozifanya ili kuhakikishia Watanzania tunapata Maendeleo kwa wakati muafaka.
Aidha amesema Rais Samia amefanya mengi Moja wapo likiwa ni pamoja na kuifanya ushirika upate heshima ukilinganisha na hapo awali.
” Tunamshukuru Mwenyezi Mungu, lakini pia tunamshukuru sana mama yetu Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa kweli ameutendea haki sana Ushirika, kwasababu dada hivi hata pembejeo huko Vijijini kila unapopita watu wanagawana pembejeo kutokana na Ushirika imara, madhubuti, hii ni kazi ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan, hatuna cha kumpatia isipokua tunadhidhi kumuombea Kwa Mwenyezi Mungu aendelee kukusimamia katika majukumu yake pamoja na kumpatia maisha marefu na afya njema” amsema Mwinyimkuu.
Awali alisema ushirika unaleta Maendeleo kwa haraka zaidi, hivyo ni vema wananchi wakaungana kujiunga na Ushirika na kwenye vyama vya ushirika, ambapo amesema wananchi watakapokuwa wameunda vikundi hivyo vitawasaidia kuwainua kiuchumi haraka zaidi.
Akizungumzia Maonyesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji 2023 yanayoendelea katika Viwanja vya Soko Jipya Wilayani Ruangwa Mwinyimkuu amesema Maonyesho ni mazuri na anawakaribisha wananchi mbalimbali kuweza kujitokeza kwa wingi ili kuweza kujifunza mengi katika Banda lao la ushirika pamoja na mabanda Mengine mbalimbali.
” Mtu alipata Madini anaweza kwenda kununua mazao nankufanya Biashara, ushirika kwanza unaweza hata mkashirikiana mkabadilishana hata mawazo kutoka Kwa !tu mmoja kwenda Kwa mwingine, maana ukiwa na mawazo ya peke Yako inawezekana Kuna kitu kimepungua upande wako, lakini ukiwa na mtu au watu wengine mtaweza kusaidiana kupeana mawazo ” amefafanua Mwinyimkuu.
Aidha amesema watu wanavyokua kwenye ushirikakunadaidia kuchochea Maendeleo kwa haraka zaidi na hatimaye kuharakisha jambo Kwa wakati na kupata mafanikio Kwa haraka zaidi ukilinganisha na mtu akiwa peke yake anakosa ushirika maana yake atakua Hana mawazo mbadala,kwani atakua na mawazo yake binafsi ambayo ni yale yale.
Hata hivyo aliwataka wananchi kuhakikisha wanajiumga kwenye vikundi na vyama vya ushirika ili kutengeneza vitu Kwa pamoja, na hatimaye kupata Maendeleo ya haraka na Kwa wakati muafaka, Kwa kile kilichodaiwa kuwa ” Umoja ni nguvu na utengaji ni dhaifu.
More Stories
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato
Wambura asikitishwa na makundi CCM Nyakato