December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Afariki kwa kunaswa na umeme akianika nguo

Na Thomas Kiani,TimesMajira Online, Singida

AMINA Mussa (57) maarufuku kwa jina la Nyamussa mkazi wa kijiji cha Musimi mkoani Singida amekufa baada baada ya ya kufariki dunia kwa shoti ya umeme akianika nguo jana asubuhi nyumbani kwakwe.

Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wamesema kuwa marehemu alipigwa na shoti ya umeme muda wa asubuhi wakati akianika nguo kwenye kamba iliyokuwa nje ya nyumba aliyokuwa akiishi.

Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Sepuka Dkt.Yessaya Mwandigo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo mesema marehemu alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa katika kituo hicho.

Amesema kuwa baada ya kutoa ajali hiyo wafanyakazi wa TANESCO walifika eneo la tukio na baada ya uchunguzi ilibainika kuwa nyaya zinazoingiza umeme kwenye nyumba hiyo ulipitia kwenye ubao ukutani usiokuwa na sapoti ulichubuka mpira wake hivyo umeme ulisambaa kwenye nyumba hiyo na kushika bati.