January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

ADEM wajipanga kutoa kozi ya Shahada ya Uthibiti ubora elimu

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

WAKALA wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) umesema kwa mwaka wa masomo 2022/23 wamejipanga kutoa kozi ya Shahada ya Uthibiti ubora elimu(bqame).

Hayo yamebainishwa katika Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu, Sayansi na TeknolojiaOfisa habari na uhusiano wa (ADEM) Veronica Luhaga amesema wadau wa elimu pamoja na walimu kwa ujumla ni vyema wakachagamkia fursa hiyo.

Amesema kwa walimu wanaotaka kufanya udahili wa shahada ya uthibiti ubora wa elimu (bqame) ni vyema wakatembelea tovuti ya chuo ya www.adem.ac.tz.

“Kwa mwaka huu wa masomo wa 2022/2023 tunatarajia kutoa kozi ya Shahada ya uthibiti ubora wa elimu (bqame)”amesema Luhaga.

Aidha aliwataka wadau wa elimu na walimu pamoja kujitokeza katika maonesho hayo na kutembelea katika banda lao ili waweze kujua mambo mbalimbali yanayohusu Adem.

Akitaja kozi wanazozitoa adem ni pamoja na udahili wa wanafunzi wa Diploma ya uongozi na usimamizi wa elimu (dema) na diploma ya uthibiti ubora wa shule (dsqa).

Alisema jukumu kubwa la adem ni kuwaandaa walimu ili kuwa viongozi na wasimamizi wa elimu katika ngazi mbali mbali .