November 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

ADC kutekeleza yale yaliyoachwa na Nyerere

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Oline

MGOMBEA urais kupitia chama cha ADC Queen Sendiga ni vyema wananchi wakafanya maamuzi sahihi ya maendeleo kwa miaka mitano ijayo kwa kukumbuka na kutekeleza yale aliyokua akizungumza baba wa taifa hayati Julius Nyerere .

Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea urais kupitia ADC Queen Sendiga akizungumza kwenye mkutano wa hadhara Manzese jijini Dar es Salaam

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Bakhresa Manzese jijini Dar es Salaam Queen alisema kuwa kila inafika Oktoba 14 isiwe ni siku ya masikitiko bali pia iwe ni siku ya furaha kwa Watanzania kwani ni mengi ametufanyia na kutuachia.

“Nakumbuka Baba wa Taifa wakati tu tumepata uhuru wetu kutoka kwa wakoloni alisema sasa tunaenda kupigana vita nyingine na maadui watatu katika taifa letu

Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea urais kupitia ADC Queen Sendiga wakati alipowatembelea wafanyabiashara Manzese.

“Ujinga, maradhi na Umaskini, Mwalimu Nyerere alisisitiza juu ya mambo haya makuu matatu, kama na aliongeza pia kama baadae Tanzania itafanikiwa kuyamaliza basi itakua miongoni mwa nchi itakayoendela zaidi duniani” alisema.

Amesema ili kuendeleza yale aliyotuachia Nyerere ADC itahakikisha kuwa kama itaingia madarakani itahakikisha kuwa itakeleza masuala muhimu ambayo baba wa taifa alikuwa akipiga kelele kama elimu,afya na kilimo.

“Kwa kuweka mifumo bora ya utekelezaji kwa yote niliyowaelezea nawaomba tarehe 28 mkanipe kura za ndio ili mimi na nyinyi tukaingie kwenye vita ya kupigana na hawa maadui watatu ili alipolala Baba yetu wa Taifa aweze kufurahi na kuona sasa Watanzania neema imewafikia,’ alisema.

Mmgombea urais kupitia ADC Queen Sendiga (kushoto) akiwa mgombea ubunge Jimbo la Ubungo Zuwena Mohammed Abdallahna walipokuwa wakiomba kura kwa wafanyabiashara katika maeneo ya Manzese.

Pia mgombea huyo alisisitizia suala la kuboreshwa kwa miundombinu kwani katika Mkoa wa Dar es Salaam kipindi cha mvua wananchi wamekuwa wakipata usumbufu kutokana na maji kujaa na kushindwa kupitika kirahisi.

“Chagueni viongozi ambao wataenda kuhakikisha kuwa wanasimamia suala hilo na sio mihemko na kujikuta kila mwaka tupo kwenye tatizo lile lile ” alisema.

Naye mgombea ubunge Jimbo la Ubungo Zuwena Mohammed Abdallah aliwaomba wananchi wamchague ili awaletee maendeleo kwani ADC ina mkakati mzuri ambao utainufaisha nchi na wananchi kimaendeleo.

“Nitahakikisha machinjio ya masoko kwenye jimbo lake yanakuwa ya kisasa ili kuongeza ufanisi na pia wananchi watapata ajira na pia nitashughulikia kero ya miundombinu kwani Jimbo la UBungo linafikika kwa shida kipindi cha mvua,’ alisema mgombea huyo.

Alisema kuwa kama wananchi watamchangua atashughulikia miundombinu Jimbo la Ubungo kwani kuna maeneo mengi hayafikiki hasa katika msimu wa mvua” alisema Zuwena