January 13, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

ACT WAZALENDO:Ubadhirifu miradi ya Maji, unalitafuna taifa

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

CHAMA Cha ACT Wazalendo, kimeeleza kuwa ubadhirifu unaofanyika katika miradi ya maji nchini, unalitafuna taifa na kuzidi kuwaingiza wananchi katika dimbwi la Umasikini.

Kauli hiyo imetolewa na ,msemaji wa Kisekta wizara ya maji ACT Wazalendo, Ester Thomas kupitia hotuba yake iliyosambazwa kwa vyombo vya habari jana.

P

Ester amesema ,sababu kubwa ya uzalishaji wa maji kuwa chini ni uwezo mdogo wa wizara ya maji kusimamia miradi mbali mbali jambo linalochangia miradi mingi kutotoa matokeo halidsi ya fedha zinazotumika.

 “Kumekua na wimbi kubwa la ubadhillifu wa feddha ya miradi ya maji inayopelekea uucheleweshwaji wa upatikanaji wa maji katika maeneo husika hili linadhibitiswa na ripoti ya mkaguzi wa hesabu za serikali CAG za mwaka 2021,”amesema Ester

Ameongeza kuwa kumekuwa na ucheleweshwaji wa utekelezaji wa miradi ya maji safi na usafi wa mazingira wa kiasi wa shilingi bilioni 37.1 na dola za kimarekani 6.05 ambao ulikua na malengo mbalimbali ya kuwezesha upatikananji wa maji katika maeneo yaliyolengwa lakini mpaka sasa hayajakamilika.

Amesema kuwa ACT Wazalendo inaitaka serikali kuwawajibisha wakandarasi, watendaji na watumishi wote waliohusika na uzembe huu na kuwasababishia wananchi adha ya ukosefu wa maji.

Akizungumzia uchelewashaji wa miradi ya maji Vijijini,Ester amesema kaatika hotuba yake waziri wa maji kila mwaka zinaishia kutaja takwimu ndefu ya miradi iliyotekelezwa, huku kila mwaka ikitajwa miradi miradi inayochukua wastani wa miaka mitatu kukamilika.

“Hali ya ucheleweshwaji wa miradhi unathibitishwa na Mkaguzi na mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesbau za Serikali. CAG anabainisha kuwza kuchelewa kukamilika kwa mradi wa maji wenye thamani ya shilingi bilioni 7.49 kutokana na vurugu za wanancchi mfano ni kijiji cha Bacho wilayani Babati chini ya mradi wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Dareda (Dareda WSSA) ambayo illivunjwa na kuundwa BAWASA mnamo mwaka 2019,”amesema Ester

Kuhusu Upotevu wa maji katika miji mikuu ya mikoa, wilaya, miji midogo na miradi ya kitaifa Ester amesema upotevu huo una thamani ya Shilingi bilioni 332.59 na kuitaka serikali kupitia wizara ya maji kuongeza juhudi katika kusambaza miundombinu ya maji iliyo bora.

Aidha amesema  thamani ya upotevu huo kwa baadhi ya miradi iliyokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali inafikia bilioni 157 kwa mwaka wa fedha 2019/20 na shilingi bilioni 175 kwa mwaka wa fedha 2020/21.

 Amesema kuwa ACT Wazalendo inaitaka serikali kufanya ukaguzi na ukarabati wa miundombinu ya maji kama vile, mita, mabomba, matanki,kuzuia upotevu wa maji na pia kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa wananchi unafika kwa wakati.