Na Bakari Lulela,Timesmajira
CHAMA cha ACT wazalendo leo juni 9 mwaka huu kimemkaribisha na kumtangaza aliyekuwa Naibu Katibu mkuu wa Chama cha NCCR MAGEUZI Elisante Ngoma kujiunga na chama hicho.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Katibu mkuu wa ACT wazalendo Ado Shaibu amesema chama cha ACT wazalendo kinamkaribisha na kumtangaza rasmi kijana mpambanaji,mpigania haki na mtetezi wa wanyonge kujiunga na ACT wazalendo.
” ACT ni chama makini na cha kizalendo katika kuwatumikia watanzania hivyo kutokana na umakini huo kinawakaribisha vijana mbalimbali wenye moyo na utayari kwenye sekta ya uwajibikaji wa kisayansi Katika kuwatumikia watanzania,” amesema Ado

Aidha Ado amesema kuwa wanawakaribisha vijana wenye dira na utayari katika kufanya Mapindizi ya kidemokrasia ambapo chama cha ACT wazalendo kina mipango mingi ya kukipeleka chama mbele kwa maslahi Mapana ya Taifa kwa raia na wananchi wa Tanzania.
Hivyo ACT Wazalendo inafanya uchambuzi wa kina na kubaini nani ni nani na anafanya Nini katika kulitumikia Taifa lake, ambapo wapo vijana wenye ndoto kubwa za kufanya mambo makubwa katika Taifa hili amesema hawa wanakaribishwa sana ACT wazalendo.
Kwa upande wake aliyekuwa Naibu Katibu mkuu Taifa wa NCCR MAGEUZI ,Elisante Ngoma amesema kuwa amefurahi kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo ambapo chama hicho kina dira na mbinu mbalimbali za kuliongoza Taifa na watu wake.
Ameendelea kuwa ACT imejipanga vema katika hata kati za kuelekea uchaguzi mkuu, ambapo viongozi Wake ni mahiri katika kuinua uchumi na kupambana na fursa mbalimbali za maendeleo ya nchi yetu.Elisante alieleza kuwa Utawala wa Chama cha Mapinduzi (CCM) hakiwajali wananchi katika masuala ya afya na elimu na ajira ambapo ACT wazalendo wanaonekana kuwajali na kuwatumikia wananchi katika siku zijazo.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi