*Ina vipaumbele Saba ikiwemo ajira milioni 12
*Kujenga uchumi wa kujitegemea
Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online-Dar
Chama cha ACT-Wazalendo,kimezindua ilani yake yenye vipaumbele saba kuelekea uchaguzi mkuu kikiwa hakina mgombea wa kiti cha Urais,huku kikiahidi kuzalisha ajira mpya milioni 12 kwa wananchi pamoja na kujenga uchumi wa kujitegemea .
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Utekelezaji wa Ilani wa chama cha ACT-Wazalendo ambaye ni mgombea Ubunge Jimbo la Segerea kupitia chama hicho, Emmanuel Vula,wakati wa uzinduzi wa ilani yao.

“Katika vipaumbele hivyo saba chama chetu kikingia madarakani kitazalisha ajira mpya milioni 12 na kujenga uchumi wa kujitegemea usiotegemea mikopo na misaada kwa kufanya shughuli za maendeleo na kuleta ustawi wa watu,”amesema Vula.
Amesema kipaumbele kingine cha ilani hiyo ni kufufua na kujenga viwanda vipya vitakavyomilikiwa na wazalishaji vijijini na kuhakikisha angalau asilimia 85 ya malighafi ya viwanda vya ndani inatokana na wazalishaji wa ndani.
Pia kulinda haki ya wafanyabishara ndogo ndogo kwa kuruhusu kufanya biashara katika maeneo ya mji na maeneo ya mikusanyiko ya watu.
“Tutajenga nyumba 500,000 katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa ajili ya watumishi wa umma ,wazee na watu wenye ulemavu pamoja na watu wenye hali duni na kuhakikisha watanzania wanaishi kwenye nyumba za kisasa na ujenzi wake unakuwa nafuu,”amesema.


More Stories
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina
Kihongosi: Msigombane kwa itikadi za vyama