December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Zitto Kabwe

ACT Wazalendo waanza mchakato kuwapata wagombea ngazi zote

Na Mwandishi wetu,TimesMajira,Online

CHAMA cha Act Wazalendo kimeanza maandalizi ya Mkutano Mkuu wa kupitisha wagombea wa ngazi mbalimbali kwa ajili ya kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba, mwaka huu.

Kamati Kuu ya ACT Wazalendo inakutana leo jijini Dar es Salaam kwenye kikao cha maandalizi ya Mkutano Mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti 5, mwaka huu.

Chana hicho kimejidhatiti kusimamisha wagombea katika ngazi zote za urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mgombea urais wa Zanzibar, wawakilishi, wabunge na madiwani.