January 26, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic akishangilia na Franck Kessie baada ya AC Milan kutoka nyuma na kuichapa Juventus 4-2 katika mchezo wa Serie A usiku wa jana Uwanja wa Giuseppe Meazza Jijini Milan.

AC Milan yaichapa Juventus 4-2

MILAN, Italia

WACHEZAJI wa Juventus wamejikuta wakipigwa butwaa baaada ya kukubali kichapo cha goli 4-2 dhidi ya AC Millan katika mchezo wa Ligi Kuu Italia Serie A, iliyopigwa kwenye dimba la San Siro jijini Milan.

Mabao ya AC Milan yalifungwa na Zlatan Ibrahimovic dakika ya 62, Franck Kessie dakika ya 66, Rafael Leao dakika ya 67 na Ante Rebic dakika ya 80, huku magoli ya Juventus yakitiwa kimiani na Adrien Rabiot dakika ya 47, Cristiano Ronaldo dakika ya 53.

Kwa matokeo hayo yanaifanya AC Milan kupanda mpaka nafasi ya 5 ikifikisha pointi 49 huku Juventus akisalia nafasi ya 1 akiwa na pointi 75. Hii inakuwa ni comeback bora zaidi tangu kurejea kwa serie A msimu huu.