Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
ABDUL Nondo ametangaza nia ya kuwania kugombea Jimbo la Kigoma Mjini,kupitia Chama Cha ACT-Wazalendo.
Nondo amesema kuwa hiyo ni demokrasi ya kila Mtanzania ya kujitokeza kuniwa jimbo lolote na kuchukua na kurejesha fomu.
Amesema kuwa hatua ya pili kupitishwa au kutopitishwa na vikao vya chama ni hatua ya ni tatu kidemokrasia,kuingia ulingoni kupeperusha bendera ya chama baada ya kuteuliwa na vikao vya chama.
Amesema kuwa baada ya kazi na majukumu makubwa aliyoyafanya Zitto Kabwe katika kipindi cha miaka mitano ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Kigoma mjini,wakazi wa Jimbo la Kigoma mjini bado wana fursa ya kuendelea kuchagua mbunge mwenye uwezo na ujasiri wa kuisimamia ,kuikosoa na kuishauri Serikali kikamilifu kwa maslahi ya wananchi.
“Wakazi wa Jimbo la Kigoma mjini bado wana fursa ya kuendelea kuchagua Mbunge mwenye uwezo wa kuwasemea na kuwatetea muda wote panapotokea uonevu na dhulma dhidi ya wananchi,” amesema.
“Nitaelezea vipaumbele vyangu na malengo ya kipi nitakifanya pale ambapo michakato ndani ya chama itakamilika (Uteuzi wa mgombea),ikiwa kama nitateuliwa na chama chetu.Ila kwa ujumla Jimbo la Kigoma mjini kwa muda mrefu kumekuwa na changamoto ya mzunguko wa kifedha kutokana na uchache wa shughuli za kiuchumi na ndani ya miaka mitano.
“Mbunge anayemaliza muda wake Zitto amekuwa akipambana kutatua Changamoto hii kwa kuanzisha miradi ya kimkakati kukuza shughuli za kiuchumi na mzunguko wa fedha katika Jimbo la Kigoma mjini ,hivyo haya ni mambo muhimu ambayo nitayaendeleza ,kuyasimamia na kuanzisha miradi mingi zaidi kwa niaba ya maendeleo ya jimbo.
More Stories
CCM hakuna kulala, Nchimbi atua Tabora kwa ziara ya siku mbili
Kongamano la Uwekezaji na Biashara lafunguliwa Pwani
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi