Na Heri Shaaban,Timesmajiraonline,Temeke
CHAMA cha Alliance For Afrika Farmers Party(AAFP),kimempitisha Kunje Ngombare Mwiru, kugombea urais katika uchaguzi Mkuu Tanzania Bara.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi wa chama cha AAFP Katibu wa chama hicho Rashid Ligania,amesema chama chao kina vikao vitatu kwa mwaka,mkutano mkuu na mkutano wa Halmashauri kuu kwa ajili ya kuchagua mgombea urais wa Tanzania bara na Visiwani wapiga kura jumla yake 118 washiriki katika mkutano huo 97 ambao wamepiga kura.
“Chama chetu leo kimepitisha Kunje Ngombare Mwiru kwa kupata kura 76 zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu na mgombea mweza wa Tanzania Bara Chum Juma Abdalah aliyepata kura 76,”amesema Rashid.

Katibu wa AAFP amesema kwa upande wa Tanzania Visiwani nafasi ya mgombea urais iligombewa na Mwenyekiti wa chama hicho cha AAFP Soud Saud Soud, ambapo alikuwa mgombea pekee wapiga kura walipiga kura za ndio au hapana, hivyo kupelekea kukosa sifa za kuchaguliwa kura za ndio zilikuwa 19 na kura za hapana 77 zilizoaribika kura 2.
Kwa upande wake Msajili Msaidizi wa vyama vya siasa nchini Sisty Nyahoza amesema kutokana na mgombea urais Tanzania Visiwani kukosa sifa za kuchaguliwa taratibu zinatakiwa zifuatwe waende wakalete majina mapya Kamati Kuu ya Zanzibar kwa ajili ya uchaguzi mwingine kumpata mgombea urais.
Msajili wa vyama vya siasa amesema nchi ina ishi kama familia hivyo tuishi kwa upendo na kudumisha amani ambapo aliwataka Wagombea kuheshimiwa taratibu ukishinda au kushindwa kwa kuwa ukivunja sheria utavunja taratibu za nchi yetu.
Mwenyekiti wa chama AAFP ambaye ndio aliyekosa nafasi ya kugombea urais Soud Said Soud aliwapongeza wapiga kura waliompigia kura za hapana kwani hawataki chama hicho kuendelea na uchaguzi ujao atapumzika agombei tena kiti hicho.

More Stories
DC Mpogolo:DMDP kujenga barabara za urefu km 67 Ilala
Uhakiki na uchambuzi wa kazi za waandishi wa tuzo za Samia Award wafanyika kwa weledi
Wananchi Arusha wapatiwa elimu sahihi ya ununuzi na umiliki wa ardhi