March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bonnah awakumbusha vijana kupiga kura Oktoba 29,2025

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online-Dar


Mgombea Ubunge Jimbo la Segerea kupitia Chama Cha. Mapindizi (CCM), Bonnah Kamoli,amewakumbusha vijana wa vilabu vya Jogging kutoka maeneo mbalimbali jimboni humo kujitokeza Oktoba 29 Octoba mwaka huu kupiga kura katika uchaguzi mkuu.

Kamoli amesema hayo katika bonanza la vilabu vya Jogging kutoka Jimbo la Segerea wakati wa tamasha la IJA FESTIVAL SEASON 1 lililofanyika Kata ya Tabata wilayani Ilala.

“Vijana wa jimbo la Segerea nawakumbusha siku Jumatano Oktoba 29,mwaka huu kunipigia kura niweze kuwa Mbunge wenu ili niweze kuwaletea maendeleo pamoja na kumpigia kura Dkt.Samia Suluhu Hassan ili awe Rais bila kuwasahau Madiwani wanaotokana na CCM,”amesema Kamoli.

Pia amesema yeye ni mwana michezo hivyo akipata ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi na kuwa Mbunge,atahakikisha sekta ya michezo jimboni Segerea inakua pamoja na kuboresha viwanja vya michezo vyote vikiwemo viwanja vya Segerea Tototundu ,Kiwalani na Kinyerezi.

“Nitawainua vijana katika michezo kwani michezo ni afya,ajira pia ujenga uhusiano mzuri,”amesema Kamoli.

Mwenyekiti wa Umoja Wanawake UWT Taifa,Mery Chatanda,amewataka vijana kuhamasisha michezo kwa ajili ya afya na ajira pia huku wananchi wa Jimbo la Segerea kushiriki michezo mara tatu kwa siku kwa ajili ya afya yao na kuweka mwili vizuri.

Pia Chatanda,amewahimiza vijana kutumia haki yao ya msingi kupiga kura kwa kumchagua Dkt.Samia Suluhu y kwa nafasi ya Urais, Ubunge Bonnah Ladslaus Kamoli na Madiwani wanaotokana na CCM.

Kwa upande wake Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Dar-es-Salaam kutoka CCM,Richard Kasesela,amewahimiza vijana wa Jimbo la Segerea na maeneo mengine ya nchi,kutumia demokrasia yao ifikapo Oktoba 29,2025 wote wajitokeze kupiga kura kwa kufuata taratibu za nchi yao pamoja na kudumisha amani na upendo.