Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online- Iringa
MGOMBEA Mwenza kiti cha Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema endapo chama hicho kitashinda katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025,Serikali yake itajenga vituo vipya viwili vya kukusanyia na kuuza maziwa mkoani Iringa.
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Ifwagi, Mufindi Kaskazini mkoani Iringa,Septemba 24, 2025,pia amesema malambo makubwa mawili ya kunyweshea mifugo yatajengwa Mufindi Kaskazini.

Dkt. Nchimbi amesema miradi yote ya maendeleo itaendelea kuwafikia wakazi wa Mufindi Kaskazini na Mkoa wa Iringa kwa ujumla, endapo wataichagua tena CCM iweze kushika dola.
“CCM ndiyo chama pekee kinachojali, kusikiliza na kutatua kero za wananchi wake na endapo kitaingia tena madarakani.Mkoa huu wa Iringa vitajengwa vituo vipya viwili vya kukusanyia na kuuzia maziwa,”amesema Dkt.Nchimbi.
Pia amesema miradi mingine itakayofanyika katika Jimbo la Mufindi Kaskazini ni pamoja na uboreshwaji wa hospitali ya wilaya kwa kuongeza majengo ya huduma pamoja na wataalamu.
Ambapo vituo vya afya vitano, zahanati nane huku shule za msingi saba na sekondari nne pamoja na kuboresha sekta ya kilimo, mifugo na miundombinu ya barabara.
Sanjari na kuanzishwa mashamba darasa kwa ajili ya wakulima, wafugaji na wavuvi, lengo ni kuwawezesha kufanya shughuli zao kitaalamu pamoja na kuanzishwa kwa miradi mipya ya maji.



More Stories
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi