March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Matengenezo mtambo wa Ruvu Juu yakamilika

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA),imekamilisha matengenezo ya dharura ya saa 18 katika mtambo wa kusukuma maji Ruvu Juu uliopo Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani,yaliosababisha kupungua kwa huduma ya maji kwa wakazi Mlandizi hadi Kisarawe.

Akizungumzia kukamilika kwa kazi hiyo, Meneja wa Mtambo wa Ruvu Juu,Mhandisi Juma Kasekwa,amesema kazi imefanyika mchana na usiku ili kukamilisha matengenezo haya muhimu.

“Pampu zetu za kusukuma maji zilipata changamoto na kazi ya matengenezo ilianza jSeptemba 22,2025 na yamedumu kwa saa 16. Kwa sasa matengenezo yamekamilika na pampu zinaendelea kusukuma maji kama kawaida yake,”amesema Mhandisi Kasekwa.

Kukamilika kwa matengenezo haya kutaboresha huduma ya maji kwa wakazi wa Mlandizi hadi Kisarawe,maeneo ya Chalinze, Ruvu Darajani, Ruvu JKT, Vigwaza, Mabwawa, Visiga, Maili 35, Maili Moja, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe Saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege.

Pia maeneo mengine ni Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi Inn, Mbezi Kimara, Tabata Segerea, Kinyerezi, Kisukuru, Saranga, Bonyokwa, Msigani, Maramba Mawili, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, Ubungo, Magomeni, Ukonga, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Vingunguti, Gongo la Mboto, Pugu na Kisarawe.