March 8, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ajali ya gari yasababisha vifo vya masista wanne,dereva Mwanza

Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza 

 Magari mawili yamegogana na kusababisha vifo vya watu watano wakiwemo masista wanne na dereva mmoja, wilayani Misungwi mkoani Mwanza.

Akizungumza Septemba 16,2025,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,Wilbord Mutafungwa, amesema,mnamo Septemba 15,2025 majira ya saa 1.50 usiku, katika kijiji cha Bukumbi, Kata ya Idetemya,Tarafa ya Usagara, wilayani Misungwi mkoani hapa,barabara ya Usagara-Kigongo Feri, kulitokea ajali ya gari yenye namba za usajili T 852 DGP aina yaToyota Land Cruiser.

Gari hiyo ni mali ya shule ya sekondari ya Wasichana Bukumbi ikiendeshwa na dereva wa shule hiyo, Boniphace Msonola(53),ikiwa inaelekea Mwanza kutokea Kigongo Feri,ilihama barabara upande wa kulia na kugongana na gari yenye namba za usajili T 541 DCH aina ya Sino Truck,mali ya kampuni ya Nyanza

Road Works iliyokuwa inaendeshwa na dereva wa kampuni hiyo Venance Mashaka(61) ikitokea Usagara kupelekewa Kigango Feri.

Mutafungwa amesema,baada ya magari hayo kugongana yalisababisha vifo vya

watu watano waliokuwa katika gari ndogo aina ya Toyota Land Cruiser.

Ambapo katika ajali hiyo watu wanne walifariki katika eneo la ajali na mmoja ambaye ni dereva wa gari T 852 DGP aina ya Toyota Land Cruiser alifariki katika hospitali ya Bukumbi wakati akiendelea kupatiwa matibabu. 

Pia amesema,chanzo cha ajali hiyo ni

mwendokasi wa gari ndogo kwa kulipita gari lililokuwa mbele yake bila

kuchukua tahadhari kisha kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa linakuja

mbele yake.

Hata hivyo Mutafungwa amewataja waliofariki katika ajali hiyo ni Sr. Nelina Semeoni(60),Mkuu wa Shirika la Wakarmeli Wamisionari wa Mtakatifu Terezia wa Mtoto Yesu, raia wa Italia,

Sr.Lilian Kapongo(55), mkazi wa Tabora.

Mwingine ni Sr. Damaris Matheka(51) Mkuu wa shule ya sekondari ya

Wasichana Bukumbi na raia wa Kenya,

Sr. Stellamaris Muthin(48),raia wa Kenya na Boniphace Msonola(53), dereva na mkazi wa Bukumbi,Wilaya ya Misungwi.

Aidha amesema,majeruhi katika ajali hiyo ni Sr. Pauline Mipata(20), Msimamizi wa wanafunzi wa shule ya sekondari Bukumbi ambaye anaendelea na matibabu katika hospitali ya Kanda Bugando. 

“Miili ya marehemu imehifadhiwa katika

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa ajili ya uchunguzi wa kitaala. Dereva wa gari T.541 DCH, Venance Mashaka,

anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano,”amesema Mutafungwa.

Vilevile Mutafungwa ametoa wito kwa madereva kuchukua tahadhari barabarani kwa kuepuka mwendokasi pia kwa watumiaji wengine wa barabara kufuata sheria,kanuni na taratibu za usalama barabarani kwa kuchukua tahadhari za kiusalama.

Error Icon

Recipient inbox full

Your message couldn’t be delivered to kagarukimajira@yahoo.com. Their inbox is full, or it’s getting too much mail right now.

LEARN MORE

WarningThis link will take you to a third-party site

The response from the remote server was:

552 5.2.2 This message could not be delivered because the recipient’s mailbox is full. Please try again later or contact the recipient directly. See https://senders.yahooinc.com/smtp-error-codes#mailbox-full for more information

Show quoted text