March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Polisi Ruvuma wakabidhiwa magari, RC atoa maelekezo

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online -Songea

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Ahmed Abbas,ametoa wito kwa Jeshi la Polisi mkoani humo kuhakikisha wanatumia vitendea kazi walivyopewa yakiwemo magari kwa usahihi na umakini.

Wito huo ametoa kwenye hafla fupi ya kukabidhi magari 24 iliyofanyika kwenye viunga vya ofisi ya Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma.Ambapo magari hayo yaliyotolewa na Serikali kwa Jeshi la Polisi mkoani humo.

iBrigedia Jenerali Ahmed,amesema magari hayo yatapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya usafiri kwa askari wanapokuwa kwenye majukumu yao ya kila siku.

” Magari haya ili yaendelee kufanya kazi ni lazima mhakikishe mnayafanyia matengenezo kila muda wa matengenezo unapofika ili yaendelee kutumika sasa na hapo baadae,”.

Pia amesisitiza kuwa weledi ,utii ndio kiapo cha askari wanachopaswa kuishi nacho katika majukumu yao ya kila siku na si vinginevyo.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma, Marco Chilya,ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini kwa kuona umuhimu wa kutoa magari hayo ambayo katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu pamoja na shughuli zingine yatasaidia kwa kiasi kikubwa kulinda usalama wa raia wema na mali zao.

Chilya ametoa wito kwa wananchi kujenga uhusiano mzuri na vyombo vya dola ili kuendelea kudumisha amani na kusaidia kufichua wahalifu ambao wanaweza wakahatarisha uvunjifu wa amani na kwamba magari hayo yatasambazwa kwenye Wilaya zote tano za Mkoa wa Ruvuma.