March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali kutumia rasilimali za bahari kwa uchumi wa bluu

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online

SERIKALI imesema imedhamiria kutumia rasilimali za bahari na maji ya ndani kwa maendeleo endelevu ya taifa kupitia uchumi wa buluu.

Hayo yamebainishwa jijini Dar-es-Salaam Septemba 10,2025 , na Naibu Katibu Mkuu Muungano kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Abdallah Mitawi,wakati akifungua kongamano la siku mbili la kitaifa la wadau wa uchumi wa buluu .

Amesema uchumi wa buluu ni injini mpya ya maendeleo endelevu kwa nchi ikiwa ni pamoja na kukuza biashara na kuimarisha ustawi wa wananchi.

“Uchumi wa buluu unaweza kuongeza ajira, kukuza biashara na kuboresha ustawi wa wananchi,” amesema

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchukuzi,Shomari Shomari amesema maboresho ya bandari, reli na vyombo vya usafiri wa majini ni muhimu katika kuimarisha uchumi wa buluu na kuongeza ushindani wa kibiashara.

Naye Mkuu wa Chuo cha Bahari (DMI), Profesa Tumaini Gurumo,amesema kuwa chuo hicho kina jukumu la kutoa elimu, kufanya tafiti na kuzalisha wataalamu wa sekta ya bahari na mazingira ya pwani.

Kongamano hilo linafanyika kwa ushirikiano wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Uchumi wa Buluu Zanzibar na DMI, likiwa na lengo la kuweka mikakati ya kitaifa ya maendeleo ya uchumi wa buluu.