📌 Asema Wizara ya Nishati ipambane irudi na ushindi
📌 Asema Wizara ya Nishati iwe mfano kwa Wizara zingine
Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Nishati, Ziana Mlawa leo amesema kushiriki michezo mbali mbali inasaidia katika kujenga afya ya mwili na akili hivyo mtumishi anapopata nafasi ya kushiriki michezo yeyote aitumie ipasavyo pia husaidia hali itakayowajengea uwezo kujiamini zaidi ikiwemo katika maeneo ya kazi.
Mlawa ameyasema hayo alipokuwa akiwaaga watumishi wa Wizara ya Nishati watakao shiriki michezo ya SHIMIWI itakayofanyika jijini Mwanza kwanzia tarehe 1 Septemba 2025

” Pamoja na kushiriki michezo ambapo ni mbali na eneo la kazi mkumbuke mkiwa huko ni eneo la kazi nidhamu na uadilifu uwe kipau mbele mdaa wote muwapo kwenye michezo hiyo.” Amesisitiza Mlawa
Ameongeza kuwa watumishi hao wajitahidi wapate ushindi ambapo kwa ushindi huo Wizara itapata heshima njee na ndani ya Wizara

More Stories
TAMWA yakumbusha jamii kupinga ukatili wa kijinsia kuelekea siku ta wanawake Duniani
Wanawake washauriwa kuchangamkia fursa za uchumi
Aida:Wanawake wakipata haki zote itapunguza migogoro