Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Ndugu. Kailima Ramadhani leo tarehe 30 Agosti, 2025 ameongoza kikao cha wawakilishi wa vyama vya siasa kupitia na kufanya mabadiliko madogo kwenye ratiba ya mikutano ya hadhara ya kampeni za wagombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais.
Mikutano hiyo iliyoanza tarehe 28 Agosti, 2025 inaendelea hadi tarehe 28 Oktoba, 2025 kwa Tanzania Bara na tarehe 27 Oktoba, 2025 kwa Tanzania Zanzibar.
Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Madiwani kwa Tanzania Bara utafanyika tarehe 29 Oktoba, 2025.








More Stories
Dkt.Homera ahimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia
Wafanyabiashara,Wananchi tumieni bandari ya ziwa Nyasa
Madiwani wawataka wazazi kuchangia chakula mashuleni