March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shule ya Holy Land yatajwa kuiheshimisha Wilaya ya Chunya

Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Chunya

MKURUGENZI wa shule ya Awali na Msingi ya mchepuo wa kiingereza ya Holy Land iliyopo katika Mji mdogo wa Makongolosi Wilayani Chunya,Lawena Nsonda (Baba mzazi)amepongezwa kwa kuwa na maono ya kuanzisha shule ambayo imeifanya wilaya hiyo kuheshimika kwa kuwa kinara wa utoaji taaluma  iliyo bora kimkoa na kitaifa kwa shule zote za mkoa wa Mbeya za Mchepuo wa Kiingereza .

Pongezi hizo zimetolewa Agosti 28,2025 na  Mchimbaji wa Madini Maarufu katika Wilaya hiyo Masaga Kaloli  ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika mahafali ya pili ya Darasa la saba na mahafali ya tano na awali ambayo imekuwa mfano bora kwa shule  za mchepuo wa kiingereza kwa Mkoa wa Mbeya.

Kaloli amesema kuwa awali alikuwa mbishi kwenye shule binafsi kutokana na baadhi ya wazazi kudangananyana kuhusu shule za mchepuo wa kiingereza.

Aidha Kaloli amesema Moja ya vitu vilivyofanya wilaya ya Chunya kuheshimika na  wilaya hiyo kutambulika ni shule ya Holy Land  na kusema shule hiyo imekuwa ya kwanza kitaifa mara mbili mfululizo.

“Shule hii imekuwa unatuwakilisha vizuri kitaaluma kwani kuna watoto kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Arusha Katavi,Iringa, Mbeya,Mwanza na Tabora karibu maeneo yote ya nchi nzima watoto wapo hapa na hii inamaanisha kuwa watu wanafuatulia sifa za shule na hii sababu ya maono na  ubunifu mkubwa wa mkurugenzi wa shule  hii leo umetupa heshima kubwa kwa wanachunya “amesema Masaga Kaloli

Hata hivyo Kaloli amesema wanataka chunya iendelee kuwa mbio na kuwataka wawekezaji,wazawa kumpa sapoti Lawena Nsonda(Baba mzazi)na kusema mkurugenzi huyo amekuwa mfanyabiashara wa muda mrefu wa duka mpaka kufika hatua ya kubuni kuwa na shule iliyopo bora .

Yona Mwakalinga ni Mkuu wa Shule ya awali na Msingi ambayo ni ya Mchepuo wa Kiingereza ya Holy Land amesema kuwa shule hiyo ilianzishwa mwaka 2019 ikiwa na wanafunzi wawili na Mwalimu mmoja na Jengo moja lenye vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja lakini ilipofika mwaka 2020 shule hiyo ilipata usajili kamili kwa kwa namba EM.18174 ikiwa ni shule ya awali na Msingi na kutwa na wakati huo ilikuwa ya jumla ya wanafunzi 65.

Akielezea zaidi Mkuu huyo wa shule amesema kuwa  mwaka 2021 shule hiyo ilipata usajili wap kutoa huduma bweni kwa wanafunzi ikiwa na wanafunzi  zaidi ya 512 na mpaka Sasa kuna jumla ya wanafunzi 657.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Shule pamoja na mafanikio hayo shule hiyo amesema inachangamoto ya ukamilishaji wa ghorofa Nne kwa ajili ya madarasa,Ofisi,Mabweni na Ukumbi wa kisasa ambao hadi Sasa ujenzi wake umefikia asilimia 20,upungufu wa vitabu vya kutosha kwenye maktaba ya shule kwa ajili ya  wanafunzi kujisomea.

Aidha changamoto nyingine alitaja kuwa ni upungufu wa nyumba za walimu, ambapo  upungufu ni  nyumba tano pamoja na upungufu wa Kompyuta  640 ,kwa ajili ya somo la TEHAMA ambapo zilizopo ni 320,000,000 pia amesema fedha zinazohitajika ili kuweza kutatua changamoto hiyo ni zaidi ya Ml.380 ,na kusema kuwa kama shule wamefanikiwa kupata Mil.427,000,000.