Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
MASHINDANO ya Selous Marathon yaliyofanyika Agosti 23, 2025 kwa mara ya saba mkoani Morogoro, yameendelea kuvutia maelfu ya washiriki na mashabiki.
Miongoni mwa washiriki ni Yas na Mixx ambao walionesha taswira mpya ya ushiriki wa kitaifa kwenye michezo kama nyenzo ya kukuza utalii na afya ya jamii.
Akizungumza mara baada ya mbio hizo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, alitoa wito kwa waandaaji wa Selous Marathon kujipanga zaidi ili kuwapa nafasi na nguvu wakimbiaji wa hapa nchini waweze kutoboa kimataifa.
“Tukifanya hivi, Selous Marathon itakuwa kubwa zaidi, itavutia watalii wengi na kuiweka Tanzania kwenye ramani ya kimataifa ya mashindano ya mbio. Mimi na mkoa wa Morogoro tupo tayari kushirikiana nanyi kuhakikisha mbio za mwakani zinakuwa kubwa zaidi na zenye mvuto wa kipekee,” amesema Malima.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Yas Kanda ya Pwani Kaskazini, Abdul Ally amesema ushirikiano wao na waandaajji unaifanya Selous Marathon kuendelea kuwa tukio kubwa la kimichezo na mfano wa kuigwa nchini.
Lakini pia, kuwa chachu ya kuutangaza mkoa wa Morogoro na Hifadhi ya Selous kwa kipekee duniani.
“Kila tukio kama hili linapofanyika, linatupa nafasi ya kuendelea kutangaza urithi adhimu wa taifa letu, vivutio vyake vya utalii, na kuimarisha hadhi ya Tanzania kimataifa.
” Yas na Mixx, sisi tunaamini katika kuwekeza na kushirikiana na wadau mbalimbali kutangaza michezo na vivutio vya utalii vya hapa nchini,” amesema Abdul Ally.
Amesema, michezo si burudani pekee, bali ni chachu ya kuimarisha afya na ustawi wa mwili,Kuleta mshikamano na ushirikiano wa kijamii, na Kutangaza vivutio vyetu vya utalii ndani na nje ya Tanzania.

Aidha, amesema Yas inajivunia kuwa na teknolojia ya kisasa ya 5G na 5G iliyoenea katika mkoa wote wa Morogoro jambo linalochangia pakubwa katika kukuza sekta ya utalii ndani ya mkoa huo.
Pia, amesema kupitia mbio hizi za Selous, washiriki wanataka kuwa na uhakika wa kuwasiliana na kuonesha vivutio vyetu kwa wakati kupitia intaneti yenye kasi kitu ambacho teknolojia yetu ya 5G inafanikisha hilo.
“Licha ya Utalii na Michezo, teknolojia yetu ya 5G inarahisisha biashara, elimu kidijitali, inawawezesha wakazi kwenye masuala ya kibunifu, na inawaunganisha moja kwa moja na fursa za kitaifa na kimataifa,” amesema.
Hata hivyo Abdul amewashukuru washiriki wote kwa kujitokeza kwa wingi, na kuwapongeza wale waliopata ushindi na medali.


More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako