Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya
Wazazi,walezi na viongozi wa elimu mkoani Mbeya, wametakiwa kushirikiana kufuatilia nidhamu ya wanafunzi shuleni ili waweze kutimiza ndoto zao pamoja na kiwango cha taaluma kwa Mkoa huo kinapanda.
Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Elimu Taaluma Mkoa wa Mbeya,Mwalimu Ally Simba wakati wa mkutano wa kuwajengea uwezo maofisa usafirishaji na mama lishe ulioandaliwa na Taasisi ya Elimu ya watu Wazima ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya taasisi hiyo.
Simba amesema ili kufikia malengo ya elimu bora ipo haja ya kushirikiana kwa kufuatilia mienendo ya wanafunzi ili mkoa uendelee kufanya vizuri zaidi kitaluuma.
“Kwa upande wake Ofisa Afya wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya,Johnson Ndaro,ametumia fursa hiyo kwa kuwataka maofisa usafirishaji na mama lishe kuweka mazingira safi katika maeneo wanayofanyia kazi ili kujilinda na magonjwa ya milipuko yanayotokana na uchafu.
Mmoja wa maofisa usafirishaji, George Damson amesema,”Elimu tuliyopata itakuwa msaada na tutaendelea kubadilika, kwa sababu kila jambo na wakati wake,”.
Meshak Juma amesema kuwa maofisa usafirishaji wengi wanaingia kwenye kuendesha bodaboda bila kuwa na ujuzi wakiamini hiyo ndio kazi rahisi ya kufanikiwa kimaisha.

More Stories
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI